Mfumo wa ulimwengu wa sasa unazingatia nguvu zaidi ya haki: Mkurugenzi wa TRT
Jukwaa la 9 la TRT World limeanza mjini Istanbul, likiunganisha viongozi, wanafikra na watunga sera kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Mkurugenzi Mkuu wa TRT, Mehmet Zahid Sobaci, ameitaka jamii ya kimataifa kuwa na “maono mapya kabisa” kwa mfumo wa kimataifa, akisema kuwa miundo ya nchi zenye nguvu duniani inazingatia nguvu za kisiasa na kijeshi kuliko maadili na haki.
Akihutubia katika Jukwaa la TRT World 2025 mjini Istanbul siku ya Ijumaa, Sobaci amesema kuwa mpangilio wa sasa wa dunia hauwezi kutatua mzozo unaoongezeka duniani kwa sababu “nguvu inachukuliwa kuwa kipaumbele kuliko maadili.”
“Mpangilio wa kimataifa wa leo hauwezi kuendeleza suluhisho la migogoro inayokabiliwa nayo,” aliwaambia wajumbe.
“Tunahitaji maono mapya kabisa ili tuweze kujenga mpangilio wa kimataifa wenye haki, unaotegemea sheria na maadili.”
Akitaja ukiukaji wa haki za binadamu unaoendelea, Sobaci alikosoa jitihada za kuhalalisha mauaji ya halaiki yanayotekelezwa na Israel Gaza katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, akisisitiza kuwa Uturuki imekuwa sauti ya haki dhidi ya ukandamizaji na viwango viwili.
“Kwa miaka miwili iliyopita, mauaji ya halaiki ya Israel Gaza yamejaribu kuhalalishwa,” alisema.
“Lakini Uturuki imekuwa sauti ya haki.”
“Wakati dunia imekuwa ikishuhudia uharibifu wa kimfumo wa watu fulani, Uturuki haijakaa kimya,” amesema.
Jukwaa la 9 la TRT World limeanza mjini Istanbul, likiwaleta pamoja wanafikra na watungasera kutoka sehemu mbalimbali za dunia kujadili jinsi hali halisi za kimataifa zinavyobadilika wakati wa kutokuwa na uhakika.
Likifanyika chini ya kaulimbiu "Merekebisho ya Ulimwenguni: Kutoka Utaratibu wa Zamani hadi Uhalisia Mpya", tukio la siku mbili linaangazia jinsi mabadiliko ya uchumi, teknolojia, vyombo vya habari na sheria za kimataifa zinavyofafanua upya ulimwengu tunaoishi.
Likiandaliwa na shirika la habari la TRT, kongamano hili la kila mwaka la linatoa nafasi ya kuleta masuala ambayo hayajapawa kipaumbele na kuuliza maswali kuhusu jukumu la vyombo vya habari katika kuunda simulizi za kimataifa.