Rais wa Sudan Kusini Kiir amrejesha makamu wa rais katika mabadiliko ya baraza la mawaziri

Rais Salva Kiir hakueleza sababu za kuwatimua maafisa, na ni haki yake, kwa kuwa makubaliano ya amani ya 2018 yanampa mamlaka ya kufanya uteuzi katika ngazi ya kitaifa na kwenye majimbo.

By
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir. PICHA/ MAKTABA

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri siku ya Jumatatu, na kumteua makamu wa rais mpya pamoja na kumrejesha kwenye baraza mtoto wa rais muasisi wa nchi hiyo.

Rais aliwafuta kazi mawaziri wanne na gavana, na mkuu wa polisi katika mabadiliko ya hivi karibuni katika baraza.

Katika maagizo kadhaa shirika la habari la serikali la Sudan Kusini (SSBC), James Wani Igga amerejeshwa kama makamu wa rais ambapo alitimuliwa miezi tisa iliopita. Anamrithi Benjamin Bol Mel ambaye alifutwa wiki iliopita.

Wani Igga, mwanasisa mkongwe, pia aliteuliwa tena kuwa naibu mwenyekiti wa kwanza wa chama tawala cha SPLM.

Mabior Garang Mabior amerudi tena kwenye baraza kama waziri wa mazingira. Ni mtoto wa rais wa zamani John Garang, aliyefariki katika ajali ya helikopta 2005.