Korea Kaskazini, China zakutana, kukuza ushirikiano wa kimkakati

Kikao hicho, kilichofanyika jijini Pyongyang, kinakuwa cha kwanza wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuitembelea Korea Kaskazini toka mwaka 2019.

By
Kulingana na Wang, ni muhimu kwa pande zote mbili kuimarisha mawasiliano na uratibu kwenye maasuala ya kikanda na ya kimataifa./Picha:Wengine

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi siku ya ijumaa, wawili hao wakiazimia kukuza ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.

Kikao hicho, kilichofanyika jijini Pyongyang, kinakuwa cha kwanza wa Waziri wa Mambo ya Nje wa China kuitembelea Korea Kaskazini toka mwaka 2019.

Wakati wa kikao chao, Wang alimpa mwenyeji wake salamu kutoka kwa Rais Xi Jinping, akipongeza hatua ya kisiasa iliyopigwa na Korea Kaskazini.

“Tukikabiliana na hali inayoendelea kwa sasa ulimwenguni, ni vyema kwa Korea Kaskazini na China kuimarisha ushirikiano, ulinzi na hata maslahi yao,” alisema Wang.

Kulingana na Wang, ni muhimu kwa pande zote mbili kuimarisha mawasiliano na uratibu kwenye masuala ya kikanda na ya kimataifa.