Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza siku ya Ijumaa kuwa limeidhinisha kimsingi tiba ya malaria kwa watoto wanaozaliwa na wachanga kwa mara ya kwanza.
Artemether-lumefantrine ni tiba ya kwanza dhidi ya malaria iliyotengenezwa mahsusi kwa ajili ya watoto wachanga.
"Kuidhinishwa huko kimsingi kunaashiria kuwa dawa hiyo inakidhi viwango vya kimataifa vya ubora, usalama na tiba," WHO imesema katika taarifa.
Kufikia sasa, watoto wachanga wamekuwa wakitibiwa na dawa ambayo inatumika kwa watoto wakubwa -- ikiwa na hatari ya kuchanganya dozi, na kuleta madhara.
"Kwa karne kadhaa, watoto wengi wamekuwa wakifariki kutokana na malaria, kuathiri afya, utajiri na matumaini katika jamii," amesema Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.
‘Hali inabadilika’
"Lakini leo hii, hali inabadilika. Chanjo mpya, vipimo, vyandarua thabiti na dawa madhubuti, ikiwemo zile mahsusi kwa ajili ya watoto, zinasaidia kuimarisha hali.
I2024, kulikuwa na maambukizi milioni 282 ya malaria na vifo 610,000 katika mataifa 80, kulingana na WHO.
Bara la Afrika ina asilimia 95 ya maambukizi na vifo, huku watoto walio chini ya miaka mitano wakiwa ni robo tatu ya vifo hivyo.
Tiba
Shirika hilo la Afya la Umoja wa Mataifa linasema mafanikio dhidi ya malaria yanakwamishwa na watu kuwa na sugu ya dawa, na ukosefu wa kutambua, pamoja na kupungua kwa misaada kutoka nje.
WHO inasema kuidhinisha kimsingi kutasaidia mipango ya manunuzi na kusaidia upatikanaji wa tiba kwa watoto milioni 30 wanaozaliwa kila mwaka kwenye maeneo yenye maambukizi makubwa ya barani Afrika.
Kote duniani, asilimia 70 ya nchi hazina mifumo thabiti ya kufuatilia masuala ya dawa, chanjo, na vipimo.
















