Shughuli za kuwaokoa waathirika waliokwama ndani ya jengo refu lililoporomoka Nairobi zaendelea

Jengo la ghorofa nyingi lililokuwa katika hatua ya ujenzi limeporomoka katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, huku idadi ya watu isiyojulikana wakiwa wamekwama chini ya kifusi.

By
Wakoaji cha kaguwa eneo la jengo lililoporomoka jijini Nairobi, Kenya. / / AP

Jengo hilo la ghorofa nyingi lililokuwa likijengwa katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, liliporomoka siku ya Ijumaa, na kusababisha idadi isiyojulikana ya watu kukwama chini ya vifusi.

Waokoaji wanaendelea kuchimba kifusi wakitafuta manusura.

Kwa mujibu wa Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, jengo hilo lilikuwa katika eneo la South C jijini Nairobi, na vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa lilikuwa na ghorofa 16.

“Maafisa kutoka taasisi mbalimbali wapo katika eneo la tukio likifuatilia hali hiyo,” Shirika la Msalaba Mwekundu wa Kenya lilisema katika taarifa yake.

Hakukuwa na maelezo ya hapo kwa hapo kutoka kwa mamlaka kuhusu chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo au idadi ya waathirika. Idadi ya vifo bado haipo wazi.

Kuporomoka kwa majengo ni jambo la kawaida jijini Nairobi, ambako mahitaji ya makazi ni makubwa na baadhi ya wajenzi wasio waaminifu hupuuza au kukiuka kanuni za ujenzi.

Baada ya majengo manane kuporomoka na kuua watu 15 nchini Kenya mwaka 2015, Ofisi ya Serikali iliamuru kufanyika ukaguzi wa majengo kote nchini ili kubaini kama yalikuwa yanakidhi viwango vya ujenzi.

Mamlaka ya Kitaifa ya Ujenzi iligundua kuwa asilimia 58 ya majengo jijini Nairobi hayakuwa salama kwa makazi.