| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Ndege kadhaa za Marekani zaanguka Kuwait, wahudumu wanusurika: wizara ya ulinzi
Televisheni ya Taifa ya Iran inasema ndege ya Marekani aina ya F15 imedunguliwa nchini Kuwait baada ya mashambulizi ya angani ya Iran.
Ndege kadhaa za Marekani zaanguka Kuwait, wahudumu wanusurika: wizara ya ulinzi
Moshi mweusi ukionekana karibu na ubalozi wa Marekani mji wa Kuwait City baada ya lile linaloaminika kuwa shambulio la Iran Machi 2, 2026. / AFP
tokea masaa 16

Ndege kadhaa za kivita za Marekani zilianguka nchini Kuwait Jumatatu asubuhi lakini wahudumu wote walinusurika, wizara ya ulinzi ya Kuwait ilisema, huku Iran ikiendeleza mashambulizi kwa siku ya tatu eneo la Ghuba.

"Ndege kadhaa za kivita za Marekani zilianguka leo asubuhi. Akithibitisha kuwa wahudumu wote wamenusurika," msemaji wa wizara ya ulinzi alisema katika taarifa, akiongeza kuwa uchunguzi unafanywa kubaini chanzo cha ajali hiyo.

"Mamlaka zimeanzisha shughuli ya uokoaji mara moja, kuwaokoa na kuwapeleka hospitali wahudumu wa ndege kwa ajili ya matibabu. Alieleza kuwa hali zao zimeimarika," taarifa iliongeza.

Kulingana na mwandishi wa TRT World mjini Tehran, Televisheni ya Taifa ya Iran inasema ndege ya Marekani aina ya F15 ilidunguliwa nchini Kuwait baada ya kushambuliwa na mifumo ya ulinzi ya angani ya Iran.

Mapema leo, video katika mtandao wa kijamii, iliyosambazwa, inaonesha kile inachoonekana kuwa ndege ya kivita ya Marekani aina ya F-15 ikiwa imeanguka nchini Kuwait, huku mamlaka zikiwa hazijathibitisha rasmi.

Pia inadaiwa kuwa ndege hiyo ilidunguliwa kwa “bahati mbaya” na kwamba rubani alinusurika.

Video hizo zinajumuisha zile zinazodaiwa kumuonesha rubani, ambaye anashuka kwa kutumia mwavuli, akipelekwa katika gari la raia.

CHANZO:TRT World and Agencies