| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Pakistan, Uturuki zaahidi ushikiriano zaidi wa ulinzi huku maafisa waandamizi wakiitembelea Ankara
Ziara hiyo ni katika jitihada za nchi mbili hizo za kudumisha uhusiano.
Pakistan, Uturuki zaahidi ushikiriano zaidi wa ulinzi huku maafisa waandamizi wakiitembelea Ankara
Ujumbe huo pia ulitembelea idara za Uturuki za Polisi, mapambano dhidi ya ugaidi, uhamiaji na mihadharati. Picha: X/@TallalPMLN / TRT World
tokea masaa 15

Waziri wa Nchi wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Talal Chaudhry amehitimisha ziara yake rasmi ya siku mbili mjini Ankara, akithibitisha azma ya nchi yake ya kuboresha ushirikiano wa kitaasisi na Uturuki katika nyanja ya ulinzi, kukabiliana na ugaidi na mihadharati, kwa mujibu wa maafisa wa serikali.

Chaudhry aliongoza ujumbe uliojumuisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani na wakuu wa vitengo muhimu vya Wizara ya Mambo ya Ndani.

Wakati wa ziara yake, upande wa Pakistan ulifanya mkutano wa pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Munir Karaloglu na maafisa waandamizi ili kuongeza ushirikiano kati ya Wizara hizo mbili za Mambo ya Ndani.

Ujumbe huo pia ulitembelea idara za Uturuki za Polisi, mapambano dhidi ya ugaidi, uhamiaji na na kukabiliana na mihadharati kwa majadiliano ya kina yenye lengo la kuimarisha ushirikiano na kubadilishana uzoefu.

Katika kipindi cha Ramadhan, Chaudhry aliwasilisha salamu kutoka kwa Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif na Waziri wa Mambo ya Ndani Mohsin Naqvi, akisisitiza msimamo wa Pakistan wa kufanya kazi kwa karibu na Uturuki kwa ajili ya amani, ulinzi na matokeo chanya.

Uturuki kwa miaka imefanikiwa kutekeleza hatua dhidi ya ugaidi na kukata makali vitisho vinavyohusiana na ugaidi nchini, hasa wale wanaotoka katika makundi kama ya Daesh na makundi ya kigaidi ya PKK — eneo ambalo Pakistan linatarajia kukuza uzoefu unaofanana, kupambana na Daesh, na makundi ya kigaidi ya Tehrik-i-Taliban Pakistan (TTP).

Ziara ya Waziri wa Nchi wa Pakistan inakuja ikiwa ni katika jitihada za nchi hizo mbili za kukuza ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Mwezi Julai mwaka jana Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Waziri Mkuu wa Pakistan Sharif wamethibitisha azma yao ya kudumisha ushirikiano katika sekta mbalimbali, ikiwemo biashara, nishati, mawasiliano na uwekezaji.

Mwezi Septemba, 2025, Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Yasar Guler aliitembelea Islamabad katika mkutano wa 16 wa Tume ya Pamoja ya Uchumi kati ya Uturuki na Pakistan, iliyoangazia ukuaji wa muingiliano wa kiuchumi.

Amesema kwamba wakandarasi wa Uturuki wamekamilisha miradi mikubwa 72 nchini Pakistan yenye thamani ya dola bilioni 3.5, huku biashara kati ya nchi hizo mbili ikizidi dola bilioni 1.4 -ongezeko la asilimia 35 kwa mwaka huo, huku kila upande ukidhamiria kufikia kiwango cha biashara cha dola bilioni 5.

Uturuki ni moja ya wasambazaji wakubwa wa silaha Pakistan, kwa mujibu wa SIPRI.