| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Kamanda wa jeshi Sudan ajiondoa RSF na kujiunga na jeshi
Kujiondoa kwa Brigedia Ali Rizqallah, maarufu Savanah, ni wa pili tangu mwezi uliopita.
Kamanda wa jeshi Sudan ajiondoa RSF na kujiunga na jeshi
Vita nchini Sudan vimefikia mkwamo baada ya zaidi ya miaka mitatu ya mapigano. Picha/Maktaba. / Reuters

Brigedia Ali Rizqallah, maarufu Savanah, amesema katika video iliyosambaa mitandaoni Jumatatu kwamba "amejiunga na utashi wa watu wa Sudan."

"Kuanzia leo, tuko upande mmoja na RSF iko upande mwengine. Sauti yangu ni sauti ya watu wa Sudan katika mikoa yote, mashariki, magharibi, kusini, na kaskazini. Sauti yangu ni sauti ya wakimbizi na waliokosa makazi," alisema.

Hakuna kauli iliyotolewa na RSF kuhusu kujitoa kwa brigedia huyo.

Savanah alikuwa ni kamanda mwandamizi RSF, ambae aliongoza mapigano dhidi ya jeshi katika mji wa Khartoum na El Fasher, mji mkuu wa jimbo la North Darfur.

Mpaka sasa hakuna taarifa ya kikosi anachokiongoza.

Huyu ni kiongozi wa pili wa jeshi kujiondoa RSF tangu mwezi jana. Mwezi April, kamanda wa RSF Al-Nur Al-Qubba nae alijitoa na kujiunga na jeshi.

Sudan imekuwa katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe tangu Aprili 2023, kati ya vikosi vya RSF na jeshi, mapigano ambayo yamesababisha vifo vya maelfu, huku takriban milioni 13 wakikosa makazi, wengine wakikimbilia nchi jirani. Nchi hiyo hivi sasa inakabiliwa na ukame ambao umesababisha janga la kibinadamu kubwa zaidi kuwahi kutokea duniani.

Soma zaidi
Rais wa Afrika Kusini aagiza hatua za kuwalinda wanawake kufuatia mfululizo wa mauaji
Misri yakana kuingilia mambo ya ndani ya Ethiopia na kuunga mkono makundi yenye silaha
Edward Kijanangoma atawazwa mfalme mpya wa Tooro
Je, Afrika itapata viti vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?
Jeshi la Polisi Tanzania laonya wanaochochea mgomo wa madereva wa mabasi
Madaktari bingwa wa Tanzania waweka kambi ya matibabu Malawi
Makamu wa Rais Tanzania ataka vijana kupewa fursa za mafunzo ya ajira
Jeshi la Sudan lapinga madai ya kuunga mkono makundi ya upinzani Ethiopia
Uchaguzi Mkuu kurejesha utulivu Sudan Kusini?
Marekani italazimika kuondoka Mashariki ya Kati: Iran
Mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu yapungua kwa karibu asilimia 90: Serikali ya Somalia
Maambukizi ya Ebola nchini DRC ni zaidi ya 8,000 tangu kuanza kwa mlipuko huo
Watoto 17 miongoni mwa wahamiaji 250 waliookolewa katika pwani ya Mauritania
Marekani kusitisha ufadhili wa sekta ya afya nchini Zimbabwe kufikia mwishoni mwa mwezi wa Septemba
Mwanamke wa kumi apatikana amefariki katika msururu  wa mauaji nchini Afrika Kusini
Qatar Airways yakopesha marubani kwa shirika la ndege la taifa la Rwanda
Wapiganaji wa RSF wahamia upande wa jeshi la Sudan baada ya kushuhudia 'maafa'
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa kwa kunyimwa viza  kiongozi wa Sudan, Burhan kuhudhuria UNGA
Jenerali wa DR Congo miongoni mwa watu 13 waliofariki katika ajali ya ndege
Afrika itapata hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa?