Bei ya mafuta yapanda Kenya huku usambazaji ukisuasua
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA), ambayo hutoa muongozo wa bei za rejareja kwa bidhaa mbalimbali kila mwezi, ilionyesha lita moja ya petroli iliongezeka kwa asilimia 16.1 hadi shilingi 206.
Kenya imepandisha bei yake ya reja reja ya mafuta kwa asilimia 24.2 huku kukiwa na ongezeko la bei ghafi na kubana mafuta yaliyosababishwa na mzozo wa Mashariki ya Kati, kwa mujibu wa Mdhibiti wa Nishati wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA), ambayo huweka kiwango cha juu cha bei za rejareja kwa bidhaa mbalimbali kila mwezi, ilionesha lita moja ya petroli iliongezwa kwa asilimia 16.1 hadi shilingi 206.97 za Kenya sawa na Dola 1.60.
Lita moja ya dizeli pia iliongezwa kwa asilimia 24.2 hadi shilingi 206.84 za Kenya, (Dola 1.60) huku mafuta ya taa yakisalia kwa shilingi 152.78.
Mdhibiti huyo alitaja gharama za bidhaa zilizoagizwa kutoka nje, ambazo alisema zimepanda kwa hadi 68.7%, ili kuhalalisha kupanda kwa bei ya rejareja.
Mwezi Machi, EPRA iliacha bei bila kubadilika, ikisema athari za vita bado hazijaathiri bei ya rejareja.
Kenya inaagiza karibu bidhaa zake zote za mafuta kutoka Mashariki ya Kati kupitia mikataba ya serikali hadi serikali na wasambazaji wa Ghuba, ikiwa ni pamoja na Saudi Aramco Trading Fujairah, ADNOC Global Trading Ltd ya Abu Dhabi, na Emirates National Oil Company Singapore Ltd.
Saa chache kabla ya bei hizo mpya kuanza kutumika Jumanne jioni, madereva walikimbilia kwenye vituo vya mafuta katika mji mkuu, Nairobi, hivyo kusababisha foleni ndefu.
EPRA pia ilisema imepunguza ushuru wa ongezeko la thamani (VAT) kwa petroli, dizeli, na mafuta ya taa kutoka asilimia 16 hadi 13% ili "kuokoa watumiaji kutoka gharama kubwa ya bidhaa za petroli kutokana na kupanda kwa bei katika soko la kimataifa."