Wataalamu waonya watoto milioni 14 wako katik hatari ya njaa DRC

Uchambuzi wa data mpya kutoka kwa Ushirikiano wa Awamu Jumuishi ya Usalama wa Chakula (IPC) iligundua kuwa watoto wapatao milioni 14—mmoja kati ya watano – watakabiliwa na viwango vya njaa au mbaya zaidi kati ya Januari na Juni mwaka ujao.

By
Maelfu ya watu nchini DRC wamelazimika kuhama makwao kwasababu ya vita / AFP

Idadi ya watoto wanaokabiliwa na viwango vya dharura vya njaa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inatarajiwa kuongezeka kwa angalau 20% ifikapo mwaka mpya kutokana na vurugu zinazoendelea, kuhama makazi na uhaba wa chakula wa msimu, kulingana na Save the Children.

Uchambuzi wa data mpya kutoka kwa Ushirikiano wa Awamu Jumuishi ya Usalama wa Chakula (IPC) iligundua kuwa watoto wapatao milioni 14—mmoja kati ya watano – watakabiliwa na viwango vya njaa au mbaya zaidi kati ya Januari na Juni mwaka ujao.

IPC ni mamlaka kuu ya kimataifa kuhusu ukali wa majanga ya njaa.

“ Vurugu zinazoendelea mashariki mwa DRC zimeacha familia bila kupata chakula, huduma za afya, na huduma nyingine muhimu, ” Greg Ramm, Mkuruhenzi wa Shirika la Save the Children. DRC.

“Kurejea nyumbani ni vigumu kwani viwango vya umaskini vinabaki juu, hasa katika maeneo ya vijijini,” Ramm aliongezea.

Miongoni mwao, karibu milioni 2.1 watakabiliwa na viwango vya dharura vya njaa, vinavyojulikana na utapiamlo mkali na hatari kubwa ya vifo vinavyohusiana na njaa.

Robo tatu ya watoto milioni 2.1 wanaokabiliwa na njaa ya dharura kote nchini wanaishi katika majimbo ya mashariki ya Ituri, Kivu Kaskazini, Kivu Kusini na Tanganyika ambako migogoro mbalimbali, pamoja na mashambulizi ya makundi tofauti yenye silaha dhidi ya raia, yaliongezeka kwa kasi mapema mwaka huu.

Hii ilisababisha kuongezeka kwa njaa, kuhama makazi, vifo vya raia na visa vya unyanyasaji wa kijinsia.

Zaidi ya watu milioni mbili wamekimbia makazi yao kutokana na ghasia nchini DRC mwaka huu.

Uhaba wa chakula una madhara makubwa kwa afya ya watoto, na kusababisha utapiamlo, kudumaa kwa ukuaji, kudhoofika kwa kinga ya mwili, na kuongezeka kwa hatari ya magonjwa.