Sudan yamteua mkuu mpya wa majeshi
Sudan imemteua Jenerali Yassir al Atta, ambaye ni naibu wa Amiri Jeshi Mkuu Abdel Fattah al Burhan, kuwa mkuu mpya wa majeshi
Sudan imemteua Jenerali Yassir al Atta, mwanachama wa Baraza linalotawala na naibu wa Amiri Jeshi Mkuu Abdel Fattah al Burhan, kuwa mkuu wa majeshi nchini humo, msemaji wa jeshi aliiambia Reuters siku ya Alhamisi.
Hatua hiyo ni muhimu sana wakati jeshi la Sudan likiwa vitani na wapiganaji wa RSF katika vita vilivyoanza miaka mitatu iliopita, na huenda ikabadilisha mkakati huku vita vikiangazia jimbo la kusini mashariki la Blue Nile.
Al Atta amekuwa jeshini kwa zaidi ya miaka 40.
Al Atta anachukua majukumu ya mkuu wa majeshi kutoka kwa mwanajeshi mwingine mzoefu Othman al Hussein, akiwa na shughuli za kisiasa chache lakini uangalizi zaidi wa vikosi vya jeshi.