tokea masaa 2
Zaidi ya tani 200 za nyama zakwama nchini Kenya kutokana na mgogoro wa Mashariki ya Kati
Wafanyabiashara wa nyama nchini Kenya wamesema wamekwama na zaidi ya tani 200 za nyama katika hifadhi kutokana na mzozo wa Mashariki ya Kati.
Waweru Kamau, ambaye ni Meneja uzalishaji katika kampuni ya Juja International Abattoirs, anasema kukatizwa kwa njia za biashara kupitia baharini na angani kumezidisha hali hiyo.
Mashariki ya Kati hadi sasa imekuwa mnunuzi muhimu wa wazalishaji wa nyama wa Kenya, huku nchi kama vile Falme za Kiarabu, Saudi Arabia, Oman, Qatar, na Kuwait zikiongoza.
Jumla ya mauzo ya nyama nchini Kenya yalipanda hadi Sh18.7 bilioni mwaka 2024 (zaidi ya dola milioni 144) ikionesha wastani wa ukuaji wa asilimia 39 kwa mwaka.
ZILIZOPENDEKEZWA














