Afrika Kusini yataka kuanza kutengeneza dawa dhidi ya Virusi Vya Ukimwi
Leseni ya kampuni nyingine ya Afrika Kusini itakuwa ya saba kwa mpango kama huo, ikiwa ni uwezo wa kuimarisha upatikanaji wa dawa na VVU.
Afrika Kusini iko mbioni kutengeneza dawa iliofanyiwa utafiti wa muda mrefu ya kinga dhidi ya VVU, lenacapavir, baada ya kukosolewa kuwa hakuna kampuni ya Afrika Kusini iliyojumuishwa wakati shirika hilo la Marekani la Gilead Sciences lilipopewa leseni ya kutengeneza dawa hizo.
Sasa Afrika Kusini inataka watengenezaji wa nyumbani kuanza mchakato ambao utaruhusu sindano ya kinga dhidi ya VVU mara mbili kwa mwaka nchini humo, kama njia ya kuleta utengenezaji katika eneo lililokumbwa zaidi na tatizo hilo.
Serikali inafanya kazi na washirika wa kimataifa kuona ni kampuni gani itafanya nao kazi yenye uwezo wa kutengeneza dawa kwa uhakika, madhubuti na kwa bei nafuu. Kampuni itakayochaguliwa itapendekezwa kwa Gilead ipewe leseni.
Gilead, kampuni ya kutengeneza dawa ya Marekani, ilitoa leseni sita mwaka 2024 kwa mashirika la India, Misri, na Pakistan kutengeneza na kusambaza dawa kwa mataifa 120 yenye uchumi wa kati, ikiwemo Afrika Kusini. Wamekosolewa kwa kutojumuisha kampuni ya Afrika Kusini katika mpango huo.
Upatikanaji wa dawa
Kupewa leseni kwa kampuni ya Afrika Kusini itakuwa ya saba katika mpango, na kuimarisha upatikanaji wa dawa ambao wataalamu wa masuala ya VVU wanasema utasaidia katika kumaliza tatizo la ugonjwa huo wa miaka 44 kwa kupunguza idadi ya maambukizi mapya.