| Swahili
UTURUKI
2 dk kusoma
Erdogan na Meloni wajadili kuimarisha ushirikiano wa ulinzi kabla ya mkutano wa NATO jijini Ankara
Rais wa Uturuki amesema nchi yake inalenga kuimarisha ushirikiano na Italia, hususan katika sekta ya ulinzi, kabla ya mkutano wa viongozi wa NATO utakaofanyika nchini jijini Ankara, Uturuki.
Erdogan na Meloni wajadili kuimarisha ushirikiano wa ulinzi kabla ya mkutano wa NATO jijini Ankara
Uturuki kuimarisha ushirikiano na Italia katika nyanja zote, hasa sekta ya ulinzi, alisema Erdogan. / / AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amezungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Italia, Giorgia Meloni, ambapo walijadili uhusiano wa mataifa mawili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika siku ya Ijumaa, Erdogan alisema Uturuki inaendelea kuimarisha ushirikiano na Italia katika nyanja zote, hasa sekta ya ulinzi, na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua mpya za kuendeleza zaidi uhusiano kati ya mataifa hayo mawili, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki kupitia mtandao wa X.

Aidha, Erdogan alisema Uturuki inatarajia mkutano wa viongozi wa NATO utakaofanyika wiki ijayo jijini Ankara utaimarisha mshikamano na umoja wa nchi wanachama wa muungano huo.

Meloni anatarajiwa kushiriki katika mkutano huo.

Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa NATO utafanyika Ankara tarehe 7–8 Julai, ukitarajiwa kuhudhuriwa na viongozi 52 kutoka nchi 32 wanachama wa muungano huo pamoja na nchi tisa zilizoalikwa.

Ushirikiano unaozidi kuimarika

Biashara kati ya Uturuki na Italia ilifikia Dola za Marekani bilioni 32.2 mwaka 2024, hali iliyozifanya nchi hizo kuweka lengo jipya la kufikia Dola bilioni 40 katika mkutano wao uliofanyika mjini Roma mwezi Aprili 2025.

Italia iliendelea kuwa moja ya masoko makubwa ya bidhaa za Uturuki, huku mauzo ya nje ya Uturuki kwenda nchini humo yakifikia kiwango cha rekodi cha dola bilioni 12.4 mwaka 2025.

Ushirikiano katika sekta ya ulinzi pia umeimarika, baada ya kampuni ya Baykar ya Uturuki na kampuni ya Italia Leonardo kuanzisha ubia wa teknolojia za ndege zisizo na rubani mwaka 2025. Aidha, Baykar ilikamilisha ununuzi wa kampuni ya anga ya Italia, Piaggio Aerospace, mwezi Juni mwaka huo.

Italia pia imeendelea kuwa mshirika muhimu wa Uturuki katika sekta ya nishati kupitia Southern Gas Corridor, ambapo bomba la gesi la Trans Adriatic Pipeline (TAP) limekuwa likisafirisha gesi kutoka eneo la Bahari ya Caspian kwenda kusini mwa Italia tangu mwaka 2020.

Kwa sasa, takribani raia 50,000 wa Uturuki wanaishi nchini Italia, huku karibu watalii 740,000 kutoka Italia wakitembelea Uturuki mwaka 2025.

CHANZO:TRT World
Soma zaidi
Erdogan akiwa UNGA: Akumbushia kuhusu taifa la Palestina na kuhimiza mabadiliko duniani
Emine Erdogan ahimiza kuachana na ‘utamaduni wa kutupa vitu’ na kuelekea kwenye matumizi endelevu
Uturuki inalenga kubadilisha ahadi za hali ya hewa kuwa vitendo katika COP31: Waziri wa Mazingira
Rais Erdogan asema uhusiano wa Uturuki, Marekani lazima 'uimarike zaidi', vikwazo viondolewe
Erdogan apigia upatu mageuzi ndani ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Uhusiano wa Uturuki na Marekani unavuka mipaka ya kijeshi, asema Kilic
Ni masuala gani muhimu ambayo Erdogan wa Uturuki atawasilisha katika hotuba yake kwa UN?
Mkuu wa Intelijensia wa Uturuki kukuza ushirikiano na Libya
Rais Erdogan awasili New York kuhudhuria Mkutano wa 81 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Rais wa Uturuki Erdogan kuzuru Marekani kwa ajili ya kikao cha 81 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Mchakato wa 'Uturuki Isiyo na Ugaidi' wakaribia hatua ya mwisho licha ya uchochezi: Rais Erdogan
Njia ya nne ya kurukia ndege uwanja wa Istanbul kukuza uchukuzi, asema Rais Erdogan
Uturuki yawakamata watu 175 wanaohusishwa na utapeli  mitandaoni unaohusiana na wamiliki wa Kiisrael
Hurkus-II ndege ya kwanza kutengenezwa Uturuki kukabidhiwa Jeshi la Anga ya nchi hiyo
Uturuki na mataifa mengine yalaani shambulizi la Houthi dhidi ya Mecca
Mkuu wa Intelijensia wa Uturuki aitembelea Afghanistan
Hali ya Mlango Bahari wa Hormuz irudi kama kawaida, asema Fidan
'Asante, Uturuki' — Wasomali wanasherehekea kuimarika kwa uhusiano na Ankara
Erdogan apongeza ongezeko la ufaulu nchini Uturuki
Uturuki: msamaha wa silaha wa Marekani kwa Utawala wa Kigiriki wa Cypriot unahatarisha uaminifu