Trump: NATO inakabiliwa na 'mustakabali mbaya' iwapo washirika hawatasaidia vita dhidi ya Iran
Trump anasema kuwa anatarajia washirika wa Marekani kusaidia na katika Mlango Bahari wa Hormuz wakati Marekani ilisaidia Ukraine dhidi ya Urusi.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema NATO itakuwa na "mustakbali mbaya" iwapo washirika wa Marekani watashindwa kusaidia kufungua Mlango Bahari wa Hormuz, njia muhimu katika usafirishaji wa mafuta ambayo imefungwa na Iran.
Katika mahojiano mafupi na The Financial Times Jumapili, Trump amesema Marekani imeisaidia Ukraine katika vita na Urusi, hivyo anategemea Ulaya itasaidia katika Mlango Bahari wa Hormuz, ambao kufungwa kwake imepandisha bei ya mafuta duniani.
"Iwapo hakutakuwa na jibu au kukataliwa, nadhani itakuwa na musktabali mbaya kwa NATO," amesema Trump, ambae kwa miaka amekuwa akiukosoa muungano huo.
"Itakuwa vyema kwa watu wanaonufaika na Hormuz kusaidia kwa kuhakikisha kwamba hakuna kitu kibaya kitatokea huko," amesema Trump.
Alipoulizwa ni msaada gani anaotaka, Trump aliimbia The Financial Times kwamba anataka watu "watakaowaondoa watu wabaya katika fukwe."
Mazungumzo na Iran
Trump amesema yuko katika mazungumzo na nchi saba kuhusu kuudhibiti Mlango Bahari wa Hormuz.
Pia amesema Marekani inawasiliana na Iran lakini ametilia shaka iwapo Iran imejiandaa kwa mazungumzo ya kumaliza mgogoro.
Trump amewaambia waandishi wa habari kwamba serikali yake inazungumza na Iran, "lakini sidhani kama wako tayari."
Soko la mafuta duniani limepata athari kubwa kutokana na mapigano dhidi ya Iran na kutokuwa na uhakika lini mapigano hayo yataisha.
Bei ya mafuta ghafi imepanda ndani ya wiki mbili zilizopita kutokana na hatari za usambazaji.