| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan: Tumenuia kuwa kati ya nchi 10 bora kwenye mauzo ya zana za ulinzi
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha Roketsan jijini Ankara, Erdogan alisema Uturuki imeazimia kufikia lengo la Dola bilioni 11, ifikapo mwaka 2028.
Erdogan: Tumenuia kuwa kati ya nchi 10 bora kwenye mauzo ya zana za ulinzi
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki./Picha:AA
7 Aprili 2026

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema nchi yake inalenga kufikia mauzo ya Dola bilioni 11 katika sekta ya ulinzi, ifikapo mwaka 2028.

Kwa mujibu wa Erdogan, malengo yajayo ya Uturuki ni kutengeneza vifaa vya hali ya juu kwa nia ya kuingia kati ya mataifa 10 yenye kuuza vifaa vya ulinzi duniani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha Roketsan jijini Ankara, Erdogan alisema Uturuki imeazimia kufikia lengo la Dola bilioni 11, ifikapo mwaka 2028.

Aliongeza kuwa, miondombinu hiyo mipya, itaongeza uwezo wa kujilinda katika Majeshi ya Ulinzi ya Uturuki.

“Kwa mifumo hii, tutaweza kuongeza uwezo wetu wa kiulinzi,” alisema Erdogan.

Kulingana na Erdogan, uwezo wa Uturuki katika sekta ya ulinzi, ni wa kupigiwa mfano duniani.

“Leo hii, Uturuki ni nchi yenye kulinda anga yake. Tunafanya haya yote kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe,” alisema.

Aliongeza kuwa, Uturuki ni kati ya nchi zilizoanzisha mifumo mipya ulimwenguni.

CHANZO:AA