| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Erdogan: Tumenuia kuwa kati ya nchi 10 bora kwenye mauzo ya zana za ulinzi
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha Roketsan jijini Ankara, Erdogan alisema Uturuki imeazimia kufikia lengo la Dola bilioni 11, ifikapo mwaka 2028.
Erdogan: Tumenuia kuwa kati ya nchi 10 bora kwenye mauzo ya zana za ulinzi
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki./Picha:AA

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema nchi yake inalenga kufikia mauzo ya Dola bilioni 11 katika sekta ya ulinzi, ifikapo mwaka 2028.

Kwa mujibu wa Erdogan, malengo yajayo ya Uturuki ni kutengeneza vifaa vya hali ya juu kwa nia ya kuingia kati ya mataifa 10 yenye kuuza vifaa vya ulinzi duniani.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha Roketsan jijini Ankara, Erdogan alisema Uturuki imeazimia kufikia lengo la Dola bilioni 11, ifikapo mwaka 2028.

Aliongeza kuwa, miondombinu hiyo mipya, itaongeza uwezo wa kujilinda katika Majeshi ya Ulinzi ya Uturuki.

“Kwa mifumo hii, tutaweza kuongeza uwezo wetu wa kiulinzi,” alisema Erdogan.

Kulingana na Erdogan, uwezo wa Uturuki katika sekta ya ulinzi, ni wa kupigiwa mfano duniani.

“Leo hii, Uturuki ni nchi yenye kulinda anga yake. Tunafanya haya yote kwa kutumia rasilimali zetu wenyewe,” alisema.

Aliongeza kuwa, Uturuki ni kati ya nchi zilizoanzisha mifumo mipya ulimwenguni.

CHANZO:AA
Soma zaidi
Uchokozi' wa Israel lazima ukomeshwe kwa amani ya Mashariki ya Kati: Rais wa Uturuki Erdogan
Erdogan atoa wito wa ushirikiano kati ya nchi za Turkic katika ulinzi, AI na usalama wa mtandao
Marais wa Uturuki na Uzbekistan wajadili ushirikiano wa ulinzi na biashara mjini Turkistan
Rais Erdogan, aisifia Ukanda wa Kati kuwa ‘Barabara ya Silki ya kisasa’ katika ziara yake Kazakhstan
Rais wa Uturuki apewa mapokezi makubwa Kazakhstan
Uturuki yapinga madai “yasiyo na msingi kabisa” ya kuingilia siasa za Somalia
Rais wa Uturuki aelekea Kazakhstan kuhudhuria mkutano wa viongozi wa nchi za Turkic
Uturuki yakana madai ya kuingilia siasa za ndani za Somalia
Uturuki iko tayari kuanzisha mazungumzo ya moja kwa moja na Armenia: afisa
Marekani na Iran zinaonyesha “nia” ya kusitisha vita, amesema Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki
Erdogan: Uturuki ililinda mnyororo wa usambazaji wa chakula licha ya migogoro ya kimataifa
Rais Erdogan: Mabadiliko ya dunia yaonesha umuhimu wa uhusiano wa karibu kati ya Uturuki na EU
FC Galatasaray yashinda taji la 26 la ligi kuu ya Uturuki na kuongeza ubingwa wao
Rais Erdogan athibitisha uungaji mkono wa Uturuki kwa usalama wa UAE
Makampuni ya ulinzi ya Uturuki yasaini mikataba ya mauzo ya nje ya karibu Dola bilioni 8
Uturuki inalenga soko la dunia la ulinzi kwa zana zake za kivita za teknolojia ya juu
Uturuki, Saudi Arabia wafanya mazungumzo ya ngazi ya juu Ankara, wajadili uhusiano, masuala ya kanda
Uturuki yazindua 'Yildirimhan', kombora la balistiki lenye uwezo wa kufika mabara mengine
Maonesho ya Uturuki ya SAHA 2026 ya ulinzi na anga yaanza jijini Istanbul
Waziri Mkuu wa Hispania aondoka Uturuki baada ya ndege yake kutua kwa dharura kutokana na hitilafu