Kasi ya kurudi kwa demokrasia nchini Somalia baada ya miaka 56
Jimbo la Somalia la Banadir, ambalo linajumuisha mji mkuu wa Mogadishu, wakazi wake kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 56 wamepiga kura katika uchaguzi.
Ingawa mchakato wa kupiga kura nchini Somalia umeanza Disemba 25, hii inaashiria zaidi ya tarehe tu ya uchaguzi.
Inaashiria hatua ya kihistoria ambayo imewawezesha wananchi kwenda kupiga kura ya moja kwa moja baada ya miongo kadhaa.
Kabla ya mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 1969, Somalia ilikuwa moja ya nchi za Afrika zilizokuwa na demokrasia na mfumo wa kisiasa.
Kati ya mwaka 1960 na 1969, nchi hiyo ilifanya uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi, bunge lilifanya kazi kwa ufanisi, na kulikuwa na makabidhiano ya amani ya uongozi wa kisiasa.
Mjadala uliopo leo kuhusu uchaguzi wa watu kushiriki moja kwa moja, ni muendelezo wa demokrasia ambayo iliachwa bila kukamilika mwanzoni mwa kipindi cha nchi hiyo kuwa jamhuri.
Jimbo la Banadir, ambalo linajumuisha mji mkuu wa Mogadishu, wakazi wake wamepiga kura Disemba 25 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 56.
Uchaguzi huu, sio tu, ushindani wa ndani, lakini pia ni hatua muhimu yenye lengo la kuimarisha mfumo wa demokrasia nchini Somalia.
Hatua hii, dhahiri inaonesha azma ya Somalia katika kuwa na mfumo wa uchaguzi wenye kujikita kwa kura ya mtu mmoja mmoja.
Katika uchaguzi huu wa serikali za mitaa, zaidi ya wagombea 1,600 kutoka vyama 20 vya kisiasa wameshiriki ili kuwakilisha wananchi katika maeneo 16 ya utawala jimbo la Banadir.
Sehemu kubwa ya wagombea walikuwa ni vijana. Hii inaonesha kwamba mustakabali wa Somalia unaendeshwa na kizazi cha vijana.
Siku ya Uchaguzi, takriban watumishi 5000 wa uchaguzi waliopewa mafunzo walikuwa katika vituo vya kupigia kura, huku vikosi vya usalama vipatavyo 10,000 vikipelekwa kuhakikisha mchakato unafanyika kwa utulivu na amani.
Waliokuwa wakisimamia katika vituo vya kura na wapigaji kura, wote walikuwa vijana wa Kisomali.
Hi inaonesha ari ya vijana wa Kisomali kwa mustakabali wa nchi yao lakini pia inaonesha imani ya Somalia ya baadae inayosimamiwa na kizazi cha vijana.
Jinsi msingi wa mchakato ulivyowekwa
Kwa miaka 56 mfululizo, raia wa Somalia walishindwa kuwachagua wale wanaowawakilisha.
Hii ni kufuatia mapinduzi yaliyofanywa na Siad Barre mwaka 1969, siasa za vyama vingi zilifikia ukomo.
Barre alisitisha kwa muda katiba na kuitawala Somalia kwa miaka mingi kupitia mfumo wa chama kimoja.
Wakati huo, raia hawakuwa na sauti yoyote, na Wasomali hawakuwa wanashiriki mchakato wa kisiasa wa kufanya maamuzi.
Wakati huo, hali hii iliyoendelea mpaka 1991, haikuleta demokrasia.
Kinyume chake, Somalia ilisambaratika kabisa, na taifa hilo likaja kujulikana duniani kama kitovu cha migogoro ya kikabila, ukame na ufukara.
Kila mji ukaingia katika himaya ya koo tofauti, makundi na wapiganaji.
Katika miaka ya 2000, huku jamii ya kimataifa ikianza kushughulikia suala la Somalia, uongozi wa mpito ukaanza kutumika. Miongoni mwa mifumo inayotumika ni uwakilishi kwa misingi ya kikoo unaojulikana kama mfumo wa 4.5, ambao unatumika hadi leo. Mfumo huu ulipendekezwa kama hatua ya muda ili kuwaleta pamoja watu wa Somalia ambao walikuwa wamegawanyika.
Kufikia 2012, kuundwa kwa Serikali kuu ya Somalia na katiba ya muda kulidhihirisha mabadiliko makubwa.
Hata hivyo, vitisho vya usalama, hasa kuwepo kwa kundi la kigaidi la Al Shabaab, kulifanya kutimiza lengo hili iwe vigumu kwa kipindi cha muda mfupi. Uchaguzi ambao raia wanashiriki moja kwa moja, ulipangwa kufanyika 2016 na 2020 lakini ukaahirishwa kutokana na sababu za kiufundi na tofauti za kisiasa.
Baada ya kcuhaguliwa tena 2022, rais Hassan Sheikh Mohamud, licha ya changamoto zote hizi, alianzisha mfumo ambao raia watashiriki kwenye upigaji kura wa serikali za mitaa na kudhihirisha dhamira ya kuendeleza mfumo huo kwa uchaguzi wa urais pia. Kwa uchaguzi huu wa Jimbo la Banadir, lengo siyo kwa uongozi wa serikali za mitaa pekee.
Unaonekana kama hatua ya kwanza muhimu ya juhudi za Somalia kumaliza zaidi ya nusu karne bila kuwa na mfumo wa demokrasia. Pia uchaguzi huo unasemekana kutimiza azama ya muda mrefu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu.
Kujenga mustakabali
Ili Somalia kuhakikisha inajenga mustakabali madhubuti na endelevu ni kuhakikisha ushirikishwaji wa moja kwa moja wa watu katika mchakato wa kisiasa.
Uchaguzi uliojikita kwa mtu mmoja mmoja, hauwakilishi tu haki ya mtu ya kupiga kura, lakini pia ni mchakato muhimu katika kuhakikisha umma una sauti katika mustakbali wake.
Ushirikishwaji huu ni muhimu katika mabadiliko ya kisiasa na kijamii ya Somalia.Mchakato wa uchaguzi unaoshirikisha watu moja kwa moja unasaidia kujenga uaminifu kati ya serikali na jamii.
Uchaguzi ulio wazi na jumuishi unaimarisha uhalali wa wale waliopo katika nafasi za utawala wakati huo huo pia, unatoa ridhaa ya jamii katika kutoa uamuzi wa kisiasa.
Kwa jamii ambayo kwa muda mrefu imetengwa katika kutoa maamuzi, mchakato huu unakuwa na ufanisi mkubwa wa kuunganisha watu na serikali.
Uhalali huu pia unaruhusu sera za kiusalama kuwa katika misingi imara zaidi ya kijamii.
Katika mapambano dhidi ya ugaidi, hatua zinazochukuliwa na serikali zinakuwa na madhubuti zaidi zinapojumuisha uungwaji mkono wa raia.
Wakati huo huo, ushiriki wa watu katika siasa unaimarisha uwezo wa serikali katika maeneo kama vile uchumi, sera za mambo ya nje na utawala.
Katika hali hii, inakuwa ni jukumu la kitaifa kwa wadau wote wa kisiasa, iwe ni katika serikali au upinzani, pia wasomi, kuunga mkono wazi wazi hatua kuelekea demokrasia.
Sauti ya ukurasa mpya
Ni utashi wa kisiasa pekee ambao unaoonesha uimara wake kutoka kwa watu ambao unaweza kuibeba Somalia kuelekea mustakbali mpya.
Ni kwa sababu hii, muda wa mashauriano ya ndani na kufanya maamuzi ya nchi katika mahema sharti umefikie kikomo.
Mpaka miaka mitatu iliyopita, Somalia ilikuwa ni nchi ambayo mabomu bado yamekuwa yakilipuko kila siku, na ugaidi na hofu ilitanda katika maisha ya kila siku.
Leo, licha ya vikwazo vyote na vitisho, hasa kutoka kwa magaidi Al Shabab, mafanikio ya kiusalama yaliyopatikana yamewezesha watu wa Somalia kutoka nje na kupata furaha ya kupiga kura moja kwa moja kwa mara ya kwanza.
Taswira hii inatoa ujumbe ulio wazi kwa wanasiasa wa Somalia.
Kwamba, watu sasa wanataka kutoa sauti, maoni na watasikika bila kupitia mtu wa kati.
Ujasiri uliooneshwa na Wasomali waliokwenda kupiga kura ni moja ya hatua madhubuti inayoweza kubadilisha mustakabali wa Somalia.
Wakati huo huo, vikosi vya ulinzi vilivyohakikisha ulinzi wa uchaguzi na Tume ya Uchaguzi ambayo ilifanikisha uchaguzi kufanyika katika mazingira yenye furaha bila matatizo wanastahiki pongezi.
Wakati huo, uelewa wa siasa zinazoendeshwa, licha ya watu, inaonesha umuhimu wa kuwa na utawala uliojikita kwa utashi wa watu.
Mchakato ulioanza katika jimbo la Banadir hautakiwi kuonekana kuwa na ukomo kwa uchaguzi wa serikali za mitaa pekee, lakini ni kipaza sauti cha ukurasa mpya ambapo uhusiano kati ya serikali na jamii unaangaliwa upya.
Mwandishi, Abdulkadir Mohammed Nour ni Waziri wa Bandari wa Somalia na amewahi kuwa Waziri wa Sheria na pia Ulinzi. Alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Ankara Kitivo cha Sayansi ya Siasa.