Rais Tshisekedi wa DRC amzawadia gari Lumumba Vea

Hatua hiyo, inakuja baada ya wachezaji wa DRC kumuomba Ras Tshisekedi ‘kumfikiria’ Lumumba Vea, wakisema kuwa ni ‘mwenzao’ wakati wa mapambano.

By
Hatua hiyo, inakuja baada ya wachezaji wa DRC kumuomba Ras Tshisekedi ‘kumfikiria’ Lumumba Vea, wakisema kuwa ni ‘mwenzao’ wakati wa mapambano.

Shabiki wa soka wa DRC Michel Nkuka Mboladinga, maarufu kama "Lumumba Vea”, amezawadiwa gari na rais wa nchi hiyo, Félix Antoine Tshisekedi kama ishara ya kuthamini mchango wake kwa timu ya taifa ya nchi hiyo.

Lumumba amepokea gari aina ya Jeep, ikiwa ni siku chache baada ya timu ya taifa ya soka ya DRC na benchi lake la ufundi kupewa zawadi ya magari na Rais Tshisekedi baada ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2026.

Akijulikana kwa mtindo wake ushangiliaji, Lumumba Vea anatajwa kuwa chachu ya mafanikio ya timu ya taifa ya nchi hiyo, hasa wakati wa fainali za AFCON 2025, zilizofanyika nchini Morocco.

Lumumba amezawadiwa gari aina ya Jepp Toyota Fortuner, siku mbili baada ya DRC kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la Dunia kwa mwaka 2026, inayoandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico.

Hatua hiyo, inakuja baada ya wachezaji wa DRC kumuomba Ras Tshisekedi ‘kumfikiria’ Lumumba Vea, wakisema kuwa ni ‘mwenzao’ wakati wa mapambano.

"Ninafarijika na zawadi hii kutoka kwa Rais Tshisekedi, nikiwa na imani kuwa siku moja ataifanya DRC kuwa moja ya nchi kubwa duniani,” alisema.