Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan siku ya Ijumaa, alifanya kumbukizi ya miaka 3 tangu kutokea tetemeko la ardhi nchini humo.
Erdogan alisema kuwa serikali imetimiza ahadi yake ya kujenga upya maeneo yaliyoathirika ndani ya muda mfupi.
“Hatutowasau ndugu zetu ambao tuliowapoteza kwenye tetemeko hilo miaka mitatu iliyopita,” alisema Erdogan kupitia mtandao wa kijamii wa Uturuki NSosyal.
“Tuliliahidi taifa letu kuwa tutaendelea kuwa na kumbukumbu zao mioyoni na akilini mwetu, kulinda yale waliyotuachia na kuirudisha upya miji yetu. Leo hii, kwa msaada wa Mungu, tumevuka changamoto hii na kuifufua miji yeti ndani ya muda mfupi katika kipindi cha miaka mitatu. Tumetimiza ahadi yetu.”
Ujumbe huo wa Erdogan uliambatana na picha mjongeo yenye kuonesha ukubwa wa athari za tetemeko hilo na hatua za ujenzi zilizofanyika.
Februari 6, 2023, tetemeko lililotokea katikati ya Kahramanmaras, lilisababisha athari kubwa kusini mwa Uturuki, ikiwemo vifo vya maelfu ya watu.




















