Binti ya Patrice Lumumba awania nafasi nyeti OIF

Kwa sasa, nafasi ya Katibu Mkuu wa OIF inashikiliwa na Louise Mushikiwabo wa Rwanda, akihudumu kwa awamu ya pili ndani ya taasisi hiyo, kabla ya mkutano wake utakaofanyika Phnom Penh, Cambodia, mwaka huu.

By
Juliana Lumumba, binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa DRC, Patrice Lumumba./Picha:Wengine

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imemuidhinisha binti wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo Patrice Lumumba, Juliana Amato Lumumba kuwania nafasi ya Ukatibu Mkuu wa Umoja wa Nchi zinazongumza lugha ya Kifaransa (OIF ).

Juliana Lumumba anawania nafasi hiyo dhidi ya Katibu Mkuu wa sasa, Mnyarwanda Louise Mushikiwabo katika uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.

Huenda uchaguzi huo ukasadifu uhasama wa kisiasa kati ya DRC na Rwanda, hususani kutokana na kinachoendelea Mashariki mwa DRC, na tuhuma za Rwanda kukiunga mkono kikundi cha waasi wa M23.

Kwa sasa, nafasi ya Katibu Mkuu wa OIF inashikiliwa na Mushikiwabo, akihudumu kwa awamu ya pili ndani ya taasisi hiyo, kabla ya mkutano wake utakaofanyika Phnom Penh, Cambodia, mwaka huu.

Kabla ya hapo, Mushikiwabo, aliwahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Rwanda, kabla ya kuingia OIF mwaka 2018.