| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jimbo la Kano Nigeria laandaa harusi ya pamoja kwa wanandoa 1,500
Gavana wa Kano alielezea mpango huo kama hatua ya kijamii inayolenga kuimarisha familia, kurejesha matumaini na kukuza maadili mema.
Jimbo la Kano Nigeria laandaa harusi ya pamoja kwa wanandoa 1,500
Kano government hold swedding for 1500 couples

Jimbo la Kano kaskazini mwa Nigeria limeandaa harusi ya pamoja kwa wanandoa 1,500, ikiwa ni sehemu ya mpango wa serikali unaolenga kuwasaidia wanawake walio katika mazingira magumu na kupunguza vikwazo vya kifedha vinavyozuia ndoa.

Hafla hiyo, iliyoongozwa na Gavana wa Jimbo Abba Kabir Yusuf, iliwakutanisha wajane na wanawake vijana kutoka maeneo 44 ya serikali za mitaa jimboni humo.

Gavana alielezea mpango huo kama hatua ya kijamii inayolenga kuimarisha familia, kurejesha matumaini na kukuza maadili mema.

Serikali ya jimbo ilitenga takriban dola za Marekani 220,000 kwa ajili ya awamu hii ya hivi karibuni ya mpango huo. Kila bi harusi alipokea naira 200,000 kama mahari, pamoja na msaada wa kifedha wa kuanzisha biashara ndogo na kuwasaidia wanandoa hao wanapoanza maisha ya ndoa.

Mpango huo si mpya Kano. Jimbo hilo limekuwa likiandaa harusi za pamoja kwa miaka kadhaa, likilenga hasa wajane, wanawake walioachwa na waume zao, na wanawake waliopata changamoto ya kuolewa tena kutokana na gharama zinazohusika.

Mamlaka zinasema mpango huo unalenga sio tu kurahisisha ndoa bali pia kushughulikia changamoto za kijamii na kiuchumi zinazowakabili wanawake walio katika mazingira magumu.

Hata hivyo, harusi hizo za pamoja zimezua mjadala kuhusu iwapo fedha za serikali zinapaswa kutumika kuwezesha ndoa; wakosoaji wakisema kuwa uwekezaji wa muda mrefu katika ajira, elimu na fursa za kiuchumi unaweza kutoa msaada endelevu zaidi kwa vijana na familia zilizo katika mazingira magumu.

Kwa serikali ya Kano, hata hivyo, mpango huo unasalia kuwa sehemu ya juhudi pana zaidi za kuimarisha taasisi ya familia na kushughulikia mambo ambayo maafisa wanayaita matatizo ya kijamii yanayohusiana na umaskini pamoja na kuvunjika kwa mifumo ya familia.

CHANZO:TRT Afrika and agencies
Soma zaidi
Aliyekuwa afisa wa ujasusi Uganda arejeshwa Marekani kukabiliwa na mashtaka ya magendo
Mlipuko wa ugonjwa wa kimeta waua viboko 46 na tembo wanane nchini Zambia
Mwenge wa Olimpiki wawasili Senegal kwa ajili ya Olimpiki barani Afrika
Putin anaunga mkono juhudi za Afrika za kutaka mageuzi katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Niger yamteua mkuu mpya wa jeshi baada ya jaribio la uasi lililozimwa
Mfalme Oyo Nyimba kuzikwa leo kwa mujibu wa mila na desturi
Putin na Ramaphosa wajadili uhusiano kati ya Urusi na Afrika Kusini katika mkutano wa BRICS
Rais wa Zimbabwe Mnangagwa atangaza siku yake ya kuzaliwa kuwa sikukuu ya kitaifa
Bunge la Nigeria lasitisha safari za wajumbe wake Afrika Kusini kufuatia vurugu dhidi ya wahamiaji
Uchaguzi wa Nigeria 2027: Tinubu vs Atiku
Algeria yaizuia UAE kutumia anga yake baada ya kusitisha uhusiano wa kidiplomasia
Mahakama yakataa ombi la Lissu kumuita Rais Samia kutoa ushahidi
Algeria yasitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na UAE
Ufalme wa Uganda wamteua mtangazaji wa televisheni kumrithi Mfalme Oyo Nyimba
Mufti Mkuu Tanzania atoa wito kwa Waislamu kufunga siku tatu kuomba kuepushwa na madhara ya El Nino
Umoja wa Mataifa wapongeza makubaliano ya Libya kuelekea katika uchaguzi
Putin amuambia Trump: Urusi haina nia ya kuzishambulia nchi za Ulaya
Wahamiaji zaidi ya 1,000 waokolewa pwani ya Afrika magharibi ndani ya wiki moja, MSF inasema
Ghana yasema imetumia $4.37 milioni kuwarudisha raia wake nyumbani kutoka Afrika Kusini
Waburundi waomba nyaraka za kusafiria kufuatia operesheni dhidi ya wafanyabiashara wa kigeni Kenya