Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki akutana na wanadiplomasia wa OIC mjini Ankara, asisitiza umoja

'OIC ina mchango mkubwa katika kuleta haki ya dunia na kuhakikisha hatua za pamoja za ulimwengu wa Kiislamu katika migogoro ya kibinadamu na kisiasa,' amesema Hakan Fidan.

By
Futari ilifanyika katika hoteli katika mji mkuu. / Wengine. / Others

Waziri wa Uturuki wa Mambo ya Nje Hakan Fidan amekutana wakati wa iftar mjini Ankara na mabalozi na waangalizi wa nchi wanachama wa nchi za Jumuia ya Ushirikiano wa Mataifa ya Kiislamu (OIC), pamoja na taasisi za OIC zilizopo nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa vyanzo wa kidiplomasia, chakula hicho cha usiku cha futari kilikuwa katika hoteli iliyopo mjini Ankara siku ya Jumatano.

“OIC ina mchango mkubwa katika kuleta haki ya dunia na kuhakikisha hatua za pamoja za ulimwengu wa Kiislamu katika migogoro ya kibinadamu na kisiasa,” amesema Hakan Fidan kupitia mtandao wa kijamii.

Amesema kuwa Uturuki itaendelea kuchangia katika kazi za Jumuia hiyo kama mwenyekiti wa Tume ya Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC.

“Natumai mwezi huu mtukufu utaleta amani na utulivu kwa binadamu wote, na natoa shukrani zangu kwa mabalozi kwa kushiriki kwao," aliongeza.