| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Uganda yathibitisha maambukizi mapya ya Ebola
Hadi kufikia sasa, ugonjwa huo umeshaua watu wawili, akiwemo mtoto wa miaka minne nchini humo.
00:00
Uganda yathibitisha maambukizi mapya ya Ebola
Siku ya Jumatatu, Umoja wa Mataifa ilianzisha mpango wa kuchangisha Dola Milioni 11.2 kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo baada ya Marekani kusitisha utoaji wa misaada ya kibinadamu. / AFP

Maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ebola yameripotiwa nchini Uganda, huku jumla ya idadi ya wagonjwa ikifikia 12 kuanzia mwezi Januari.

Licha ya mamlaka za Uganda kusisitiza kuwa zimeweza kudhibiti maradhi hayo, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Barani Afrika (Africa CDC), kimesema siku ya Alhamisi kuwa wameweza kugundua maambukizi mapya.

Hadi kufikia sasa, ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu wawili, akiwemo mtoto wa miaka minne.

Vile vile, watu wapatao 69 ambao wanahisiwa kukutana na walioambukizwa wanaendelea kuangaliwa kwa karibu,” amesema afisa mwandamizi wa CDC Ngashi Ngongo.

Siku ya Jumatatu, Umoja wa Mataifa ulianzisha mpango wa kuchangisha dola milioni 11.2 kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo baada ya Marekani kusitisha utoaji wa misaada.

Kwa sasa, hakuna chanjo iliyothibitishwa ya ugonjwa wa Ebola.

Ugonjwa wa homa ya Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya ebola. Ugonjwa huu ni miongoni mwa magonjwa ya milipuko yajulikanayo kama homa za virusi vinavyosababisha kutoka damu mwilini.

CHANZO:REUTERS