| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Macron awasili Cyprus kujadili masuala ya amani
Rais Macron, alitarajiwa pia kuitembelea manowari hiyo ijulikanayo kama Charles de Gaulle, jumatatu mchana, ikiwa imetia nanga katika eneo la pwani ya Crete.
Macron awasili Cyprus kujadili masuala ya amani
Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron./Picha:Wengine
tokea masaa 2

Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amewasili nchini Cyprus siku ya Jumatatu kujadilia masuala ya amani, huku nchi yake ikituma meli za kivita katika bahari ya Mediterania, katikati ya mgogoro wa Marekani-Israel dhidi ya Iran.

Mara tu baada ya kuwasili jijini Paphos mapema Jumatatu, Macron alipata wasaa wa kukutana na Rais Nikos Christodoulides na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis kwa ajili ya mazungumzo.

Cyprus, ambayo ni mwanachama wa Umoja wa Ulaya, ililengwa na ndege nyuki za Iran wiki iliyopitia, hatua iliyomlazimu Macron kutuma manowari yake ya kivita katika kisiwa hicho.

Rais Macron, alitarajiwa pia kuitembelea manowari hiyo ijulikanayo kama Charles de Gaulle, jumatatu mchana, ikiwa imetia nanga katika eneo la pwani ya Crete.

Aidha, Macron amedai kufanya mazungumzo na viongozi wenzake wa Marekani na Iran siku ya Jumapili, kabla ya safari yake ya Cyprus.

Hali kadhalika, Macron alifanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kuhusu hali ya usalama katika la Mashariki ya Kati na Lebanon.

CHANZO:AFP