| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
DRC yatangaza sikukuu kusherehekea kufuzu kwa Kombe la Dunia
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza Jumatano, April 1, 2026 kuwa sikukuu ya kitaifa baada ya timu yao kufuzu kwa Kombe la Dunia 2026 siku ya Jumanne
DRC yatangaza sikukuu kusherehekea kufuzu kwa Kombe la Dunia
DRC imefuzu kwa Kombe la Dunia 2026 Machi 31, 2026 baada ya kuifunga Jamaica katika hatua ya mtoano. / Reuters
tokea masaa 3

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza Jumatano, April 1, 2026 kuwa sikukuu ya kitaifa baada ya timu yao kufuzu kwa Kombe la Dunia siku ya Jumanne.

"Waziri wa Ajira na Kazi anatangazia taifa kuwa Jumatano, April 1, 2026, ni sikukuu kote nchini," mawasiliano rasmi kutoka kwa Ferdinand Massamba wa Massamba, waziri wa kazi wa DRC, yalisema siku ya Jumatano.

"Maamuzi haya ya kipekee ni ishara ya ari ya Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye pia ni kiongozi wa Serikali ya Jamhuri, inayoongozwa na Waziri Mkuu Judith Suminwa Tuluka, kuruhusu watu wa DRC kusherehekea kwa pamoja,utashi, na fahari ya taifa," taarifa hiyo iliongeza.

Siku ya Jumanne, mashabiki wa soka waliingia katika barabara za mji mkuu, Kinshasa, na kucheza usiku mzima kwenye mvua baada ya DRC kufuzu kwa Kombe la Dunia mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 52.

'Tulijituma'

Mchezaji wa safu ya ulinzi Axel Tuanzebe, ambaye anacheza katika timu ya Ligi Kuu ya England ya Burnley, alikuwa shujaa kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamaica baada ya muda wa ziada nchini Mexico nchini Jumanne.

Taifa hilo la Afrika ya kati litakabiliana na Ureno, Colombia na Uzbekistan katika kundi K Marekani ya Kaskazini mwaka huu.

Katika fainali za 1974 Ujerumani Magharibi, timu hiyo ilijulikana kama Zaire na ilifungwa na Uskochi, Yugoslavia na Brazil.

"Tulijituma, kwenye mvua!" alieleza Beni Ile, shabiki wa mjini Kinshasa ambaye mabega yake yalilowa maji akiwa na bendera ya DRC. "Tumekuwa tukisubiri hili kwa miaka 50. Tutakaa hapa mpaka asubuhi," aliongeza.

CHANZO:TRT Afrika and agencies