Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, ameondoka kuelekea Kazakhstan kuhudhuria mkutano wa Nchi za Turkic (Mataifa yanayozungumza Kituruki) na kufanya mazungumzo ya ngazi ya juu katika mji mkuu wa Kazakhstan, kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia.
Erdogan aliagwa katika Uwanja wa Ndege wa Esenboga jijini Ankara siku ya Jumatano na Makamu wa Rais Cevdet Yilmaz pamoja na Gavana wa Ankara Yakup Canpolat.
Kwa mwaliko wa Rais wa Kazakhstan, Kassym-Jomart Tokayev, Erdogan anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa “Informal Summit of the Organization of Turkic States” katika mji wa Turkistan, pamoja na mkutano wenye mada “Astana-Ankara: Kutoka undugu hadi muungano wa kimkakati wa Eurasia,” unaolenga kuimarisha zaidi ushirikiano wa mataifa hayo mawili.
Wanaofuatana na Erdogan katika ziara hiyo ni mke wake wa Emine Erdogan, Waziri wa Mambo ya Nje Hakan Fidan, Waziri wa Elimu Yusuf Tekin, Waziri wa Ulinzi Yasar Guler, na Waziri wa Viwanda na Teknolojia Mehmet Fatih Kacir.
Waziri wa Biashara Omer Bolat, Naibu Mwenyekiti wa Chama cha AK Kursad Zorlu, Mkurugenzi wa Mawasiliano Burhanettin Duran, pamoja na Mshauri Mkuu wa Sera za Kigeni na Usalama Akif Cagatay Kilic pia ni miongoni mwa waliofuatana na Rais Erdogan.


















