| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Rais Erdogan wa Uturuki awaandalia mchapalo viongozi wa NATO na wenzi wao
Erdogan, pamoja na Mama Emine Erdogan wamekuwa wenyeji wa viongozi hao pamoja na wenzi wao, ndani ya jumba la rais.
Rais Erdogan wa Uturuki awaandalia mchapalo viongozi wa NATO na wenzi wao
Erdogan na Mama Emine, waliwakaribisha viongozi hao pamoja na wenzi wao ndani ya jumba hilo, zoezi lililotanguliwa na picha za kumbukumbu./Picha:AA / AA

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki na Mama Emine Erdogan waliwaandalia mchapalo maalumu, viongozi wanaohudhuria mkutano wa 36 wa NATO pamoja na wenzi wao, jijini Ankara.

Erdogan na Mama Emine, waliwakaribisha viongozi hao pamoja na wenzi wao ndani ya jumba hilo, zoezi lililotanguliwa na picha za kumbukumbu.

Bendi kutoka Jeshi la Ulinzi la Uturuki lilitumbuiza, wakati wa kukaribishwa kwa viongozi hao.

Kwa upande wake, Rais Donald Trump alionekana kufurahia tumbuizo la bendi hiyo ya Mehter.

Mkutano huo wa NATO, unawaleta pamoja viongozi 32  kutoka nchi wanachama wa umoja huo, kujadili uwezo wa bara la Ulaya kiulinzi na namna ya kuisaidia Ukraine.

Huu unakuwa mkutano wa pili kuandaliwa na Uturuki, kufuatia mkutano wa kwanza uliofanyika mwaka 2004 jijini Istanbul.

Mapema siku hiyo, Rais Erdogan alikutana na Rais Trump pamoja na Waziri Mkuu wa Canada Mark Carney na mwenzake wa Finland, Alexander Stubb.

Siku ya Jumatano, Rais Erdogan anatarajiwa kuhutubia mkutano huo.

CHANZO:AA