NATO yatungua kombora la Iran lililokuwa limeelekezwa Uturuki

Uturuki imesema kuwa itaendelea na jitihada za kulinda usalama wa nchi na kutafuta amani.

By
Hali kadhalila, Uturuki iliongeza kuwa itaendeleza majadiliano na NATO na washirika wake./Picha:Reuters

Jeshi la anga la Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO) yamefanikiwa kutungua kombora la Iran, lililokuwa likielekea Uturuki, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki, siku ya Jumatano.

Kombora hilo, lilitunguliwa nje ya anga la Uturuki, baada ya kuvuka mipaka ya Iraq na Syria.

Kulingana na Wizara ya Ulinzi ya Uturuki, mabaki ya kombora hilo, yalindondoka katika wilaya ya Dortyol ndani ya mkoa wa Hatay.

Hakuna majeruhi wowote walioripotiwa katika tukio hilo.

Uturuki imesisitiza kuwa, ina uwezo wa kuimarisha ulinzi wake kikamilifu, ikisesma kuwa nchi hiyo inaunga utulivu wa kikanda.

Mamlaka pia zimeonya kuwa, tishio lolote lile litadhibitiwa, huku zikizitaka pande zote kuepuka kila aina na vitendo vitakavyochochea mgogoro huo.

Hali kadhalika, Uturuki iliongeza kuwa itaendeleza majadiliano na NATO na washirika wake.

“Tunazitaka pande zote zenye kuhitalifiana na kuachana na mambo yoyote yatakayokuza mzozo huu,” alisema Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Uturuki, Burhanettin Duran katika taarifa hiyo.

Pia aliwataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa zisizo na uhakika, kutokana na mgogoro huo.