| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Rais Erdogan: Mkutano wa NATO ulikuwa wa mafanikio makubwa
Kulingana na Erdogan, mkutano huo umefanyika katika kipindi muhimu kwa eneo la Ulaya na eneo zima la Atlantiki, hasa katika masuala ya kiusalama.
Rais Erdogan: Mkutano wa NATO ulikuwa wa mafanikio makubwa
Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki./Picha:AA / AA

Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema kuwa mkutano wa viongozi wa nchi za NATO umekamilika kwa mafanikio makubwa, akilielezea tukio hilo kuwa la kihistoria.

"Tumehitimisha mkutano wa NATO kwa mafanikio makubwa ikiwa ni miaka 22 toka tuandae mkutano wa kwanza," alisema Rais Erdogan wakati wa mkutano wa waandishi wa habari.

Kulingana na Erdogan, mkutano huo umefanyika katika kipindi muhimu kwa eneo la Ulaya na eneo zima la Atlantiki, hasa katika masuala ya kiusalama.

"Mkutano huu utatupa picha halisi ya mustakabali wetu," alisema.

Kiongozi huyo, aliongeza kuwa, Uturuki imekabiliana na migogoro ya kikanda na ugaidi kwa kipindi kirefu bila kufaidi gawio la vita baridi kama ilivyo kwa nchi nyingine za Ulaya.

"Kuna nyakati ambazo tulikuwa wapweke na kutotendewa haki. Ilitubidi kutegemea nguzu zetu wenyewe," alieleza.

Kulingana na Erdogan, juhudi hizo zimeiwezesha Uturuki kuzipita nchi washirika wa NATO katika matumizi ya ulinzi na kijeshi.

"Leo hii, tumezipita nchi nyingi katika matumizi ya kijeshi," alisema Erdogan.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa viongozi wa NATO wamepitia utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa wakati wa mkutano wa uliopita The Hague nchini Uholanzi.

CHANZO:AA