Mtanzania miongoni mwa waliohamishwa kutoka Marekani hadi Eswatini
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump uliipa Eswatini dola milioni 5.1 ili ipokee wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani.
Marekani iliilipa Eswatini dola milioni 5.1 kupokea waliofukuzwa chini ya mfumo wake mpya
sera ya uhamiaji inayohusisha kuwafukuza wahamiaji hadi nchi za tatu.
Wakazi katika mji wa Eswatini wa Matsapha wanaelezea wasiwasi wao baada ya serikali kusema imepokea watu wengine wanne waliofukuzwa kutoka Marekani, Alhamisi Machi 12, 2026.
Eswatini hivi sasa, ina jumla ya wahamiaji 9 waliohamishwa kutoka Marekani.
Wawili kati ya waliofukuzwa hivi karibuni ni kutoka Somalia, mmoja kutoka Sudan na mwengine kutoka Tanzania.
Waliowasili hapo awali, ambao walihamishiwa Eswatini mnamo Julai 2025 walijumuisha raia wa Vietnam, Cuba, Laos na Yemen.
Utawala wa Trump unalaumiwa kwa kuendeleza kile kinachoitwa ukandamizaji dhidi ya wahamiaji.
Baadhi ya wakazi wanasema hatua hiyo imeongeza hofu ya uhalifu na usalama wa umma huku wengine wakihoji lengo la raia hao wa kigeni kupelekwa nchini mwao wakati changamoto zao hatijapata utatuzi.
"Kwa nini wahalifu wanaendelea kuja nchini? Je, kuna mpango wa siri wa kutuondoa?” Simanga Myeni, mkazi aliuliza.
Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump uliilipa Eswatini dola milioni 5.1 ili ipokee wahamiaji waliofukuzwa kutoka Marekani.
Eswatini ni moja ya nchi kadhaa za Afrika ambazo zimeingia kwa kiasi kikubwa
katika mipango wa Marekani ya kupokea wahamiaji. Hata hivyo, hakuna maelezo zaidi ya makubaliano hayo.
Mahakama Kuu nchini Eswatini mwezi uliopita ilitupilia mbali kesi iliyoletwa na watetezi wa haki za binadamu wanaopinga mpango huo.
Mawakili hao wamekata rufaa.
Licha ya kutumikia vifungo vyao kwa uhalifu uliofanywa nchini Marekani, waliosalia bado wanazuiliwa gerezani huko Eswatini.