Rais Vladimir Putin wa Urusi, amesema kuwa Uturuki itaendelea kuwa mshirika wa karibu na wa kweli wa nchi yake, hasa katika maeneo ya uchumi na sera za kimataifa.
Akizungumza baada ya kukutana na Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki nchini Kyrgyzstan siku ya Jumanne, Putin alibainisha kuwa uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi hizo upo katika hali ya kuridhisha.
“Uturuki ni kati ya washirika wetu muhimu katika masuala ya kisera na kiuchumi,” alisema Rais Putin, akimshukuru Rais Erdogan.
Kulingana na Putin, Uturuki na Urusi zinaendelea kutekeleza miradi mbalimbali, ukiwemo wa Nyuklia wa Akkuyu.
“Uliweka mazingira mazuri ya kuanzishwa kwa kampuni yetu ya Rosatam,” alisema Putin.
Kulingana na Putin, Uturuki inaendelea kushuhudia ongezeko la watalii wa Kirusi, ikifikia milioni 7, mwaka 2025.
Wawili hao, walikutana katika mkutano wa ushirikiano wa shirika la Shanghai, uliofanyika jijini Bishkek.






















