| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki afanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa Qatar na Syria
Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, Fidan alikuwa na mazungumzo na waziri wa Qatar, Abdulrahman Al Thani na Asaad Hassan al-Shaibani, wa Syria.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki afanya mazungumzo na mawaziri wenzake wa Qatar na Syria
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan amefanya mazungumzo ya simu, kwa nyakati tofauti na mawaziri wenzake wa Qatar na Syria.

Kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, Fidan alikuwa na mazungumzo na waziri wa Qatar,  Abdulrahman Al Thani na Asaad Hassan al-Shaibani, wa Syria.

Wakati wa mazungumzo yake na Sheikh Mohammed, Fidan alizungumzia suala la Mlango Bahari wa Hormuz, huku akiangazia masuala ya kikanda, katika mazunguzmo yake na Shaibani.

Hata hivyo, taarifa zaidi kuhusu mazungumzo hayo hazikuweza kupatikana mara moja.

CHANZO:Anadolu Agency