| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Mamlaka ya uchukuzi Kenya yazindua ukaguzi wa lazima wa afya kwa madereva ili kupunguza ajali
Mamlaka ya Kitaifa ya Uchukuzi na Usalama (NTSA) imetangaza mfululizo wa hatua za kuimarisha usalama barabarani, haswa katika barabara kuu ikizingatia afya ya dereva na matumizi ya teknolojia.
Mamlaka ya uchukuzi Kenya yazindua ukaguzi wa lazima wa afya kwa madereva ili kupunguza ajali
Kwa mfumo huu mpya, magari yatahitaji kuweka mifumo ya kidijitali iliyoidhinishwa. /NTSA / x
tokea masaa 5

Madereva wote, hususan wale wa magari ya biashara na ya Umma (PSVs), watatakiwa kufanya ukaguzi wa afya wa lazima mara kwa mara. Ukaguzi huu unahusisha tathmini ya hali zinazoweza kuathiri ujuzi wa kuendesha gari, ikiwemo: matatizo ya kuona, changamoto za kusikia, uchovu, na magonjwa sugu, NTSA iliandika kwenye taarifa yake siku ya Jumanne, Machi 31, 2026.

Mamlaka hio ilifafanua kwamba: “Matatizo ya kuona huathiri kati ya 20–30% ya watu wazima, na hali kama kisukari huathiri 3–4%. Kukabiliana na hali hizi ni muhimu kupunguza hatari zinazohusiana na nyakati za uchovu.”

Mbali na ukaguzi wa afya, NTSA pia imetangaza kuanzishwa kwa vituo vya kupumzika kwa madereva, kuhakikisha madereva wa safari ndefu wanapata muda wa kutosha kupumzika.

Pia, Mamlaka ina mpango wa kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji wa kidijitali kufuatilia mwenendo wa madereva kwa wakati halisi. Hii itahusisha: mfumo wa ufuatiliaji, na ufuatiliaji wa GPS kufuatilia mwendo wa magari, mifumo ya breki, umakini wao, na utekelezaji wa sheria za trafiki. 

"Kwa mujibu wa Ripoti ya Hali ya Usalama Barabarani ya 2025, magari ya biashara yanazidi kuchangia ajali za barabarani. Mwaka 2024, magari ya biashara yalisababisha ajali 1,087 ikilinganishwa na 3.645 ya magari mengine," Mamlaka hio ilieleza.

Kwa mfumo huu mpya, magari yatahitaji kuweka mifumo ya kidijitali iliyoidhinishwa, ambayo itatuma data kwenye majukwaa ya ufuatiliaji ya NTSA ili kubaini mwenendo hatarishi wa madereva mapema kabla ya kutokea kwa ajali.