Iran: Hatuna mazungumzo yoyote na Marekani

Iran imesema kuwa hakuna mazungumzo yoyote kati yake na Marekani, ikionya mataifa yaliyotoa ngome za kijeshi kwa Marekani, zikichukuliwe kuwa kama maadui.

By
Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Mojtaba Khamenei./Picha:Wengine

Iran imesema kuwa haijawa na mazungumzo yoyote na Marekani, ikionya kuwa mataifa yoyote yatakayotoa ngome za kijeshi kwa Marekani, yatachukuliwa kuwa maadui wa nchi hiyo.

Akizungumza siku ya Alhamisi, msemaji wa kamati maalumu inayoshughulikia masuala ya usalama wa taifa na mambo ya nje ndani ya bunge la Iran, Ebrahim Rezaei, alitoa onyo kwa mataifa yatakayodiriki kutoa ngome za kijeshi kwa Marekani.

Kulingana na Rezai, usalama ulikuwa umeimarishwa katika kisiwa cha Kharg, huku uuzaji wa mafuta ukiendelea kama kawaida.

Hakikisho hilo linafuatia kauli ya Rais Donald Trump wa Marekani, ambaye alidai kuwa mashambulizi ya Marekani yalikuwa yameharibu kisiwa hicho.