Rais Felix Tshisekedi wa DRC akutana na mshauri wa Donald Trump wa masuala ya Afrika
Wawili hao wanatarajia kukutana Aprili 3, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi anajataria kukutana na Massad Boulos, ambaye ni mshauri wa masuala ya Afrika wa Rais Donald Trump wa Marekani.
Wawili hao wanatarajia kukutana Aprili 3, 2025.
Boulos, ambaye ana asili ya Lebanon, ni mkwe kwa Rais Trump baada ya binti wa kiongozi huyo wa marekani Tiffany, kuolewa na mtoto wa mshauri huyo wa masuala ya Afrika.
Ziara ya Boulos nchini DRC, inakuja wakati taifa hilo lenye utajiri mwingi wa madini likikabiliwa na machafuko ya kisiasa ambayo yamezidi kuongezeka katika miezi ya karibuni.
"Massad Boulos aliwasili Jumatano jioni jijini Kinshasa, tayari kabisa kukutana na Rais Felix Tshisekedi siku ya Alhamisi, alisema msemaji wa Rais wa DRC Giscard Kusema katika mahojiano yake na AFP.