| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Nigeria yawaongezea mshahara wanajeshi hadi 80%
Nyongeza inatarajiwa kuanza kulipwa kuanzia mwezi ujao.
Nigeria yawaongezea mshahara wanajeshi hadi 80%
Rais Tinubu anasema nyongeza hiyo ya mishahara ni "ishara ya kuridhishwa kwa dhati" na utendaji kazi wa jeshi.

Mishahara ya wanajeshi nchini Nigeria imeongezwa kwa asilimia kati ya 30 na 80, mshauri wa rais alisema siku ya Jumanne, huku serikali ikitaka kuhamasisha vikosi vinavyokabiliana na ukosefu wa usalama kote nchini.

Nyongeza hiyo ya mishahara kwa wanajeshi karibu 250,000 inakuja huku Nigeria ikikabiliana na kupanda kwa gharama za maisha, ikiwa ni sehemu ya mabadiliko ya Rais Bola Tinubu yenye lengo la kuimarisha uchumi na hakikisho kwa wawekezaji wa kimataifa.

Mfumuko wa bei uliongezeka hadi asilimia 30 mwaka 2024 lakini umepungua hadi asilimia 15.91 mwezi Juni, huku bei ya mafuta ikiongezeka zaidi ya mara tatu katika kipindi cha miaka minne.

Karibu asilimia 61 ya raia wa Nigeria wanaishi katika hali ya umaskini, kulingana na Benki ya Dunia , ikiwa ni ongezeko la asilimia nne tangu Tinubu alipoingia madarakani Mei 2023.

Mishahara mipya

Maafisa wawili wa jeshi waliiambia AFP kuwa askari anayelipwa mshahara wa chini kabisa ni naira 100,000 ($73) kwa mwezi.

"Maafisa walio cheo cha kanali na kuendelea watapata nyongeza ya asilimia 30 ya mshahara," Mshauri wa masuala ya habari wa Tinubu Bayo Onanuga alisema katika taarifa.

"Hii pia ni kwa Brigedia Jenerali, Meja Jenerali, Luteni Jenerali na Jenerali.

"Maafisa kuanzia cheo cha kanali hadi afisa mteule watapata nyongeza ya asilimia 50, huku nafasi ya askari hadi Sajinitaji wakipata nyongeza ya asilimia 80."

Mishahra hiyo mipya, itaanza kulipwa kuanzia mwezi Septemba, na itagharimu serikali naira bilioni 924 (karibu $678 milioni), kuanzia naira dola bilioni 660 kwa ajili ya wanajeshi, kulingana na ofisi ya rais.

CHANZO:TRT Afrika Swahili