Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki akutana na rais wa UAE Abu Dhabi
Hakan Fidan pia alifanya mazungumzo na mwenzake wa UAE kuhusu kuimarisha ushirikiano
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan akiwa katika ziara rasmi UAE. /AA
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan amekutana na Rais wa Falme za Kiarabu (UAE) Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan Abu Dhabi, kulingana na vyanzo vya kidiplomasia.
Fidan alipokelewa na Rais wa UAE ambapo walijadili kuhusu hali ya uhusiano wao, vyanzo vilisema zaidi.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki pia alikuwa na mkutano mwingine na mwenzake wa UAE, Abdullah bin Zayed Al Nahyan, kulingana na taarifa ya Balozi wa Uturuki Abu Dhabi Lutfullah Goktas.
Maafisa hao walizungumzia uhusiano wao, pamoja na njia za kuimarisha ushirikiano na kufanya kazi kwa pamoja katika maeneo mbalimbali.