Trump ataka Wasomali walioko Marekani warudi kwao

Rais wa Marekani, Donald Trump ametoa wito kwa Wasomali wanaoishi Marekani warudi wakarekebishe nchi yao.

By
Trump kwa miaka kadhaa amekuwa akimkosoa Mwakilishi wa Bunge la Marekani Ilhan Omar, ambaye alihama kutoka Somalia mwaka 1995 akiwa mtoto. / / Reuters

Rais Donald Trump siku ya Jumanne alisema hataki wahamiaji wa Kisomali nchini Marekani, akisema wakaazi wa nchi hiyo iliyoharibiwa na vita mashariki mwa Afrika wanategemea sana malipo ya serkali ya Marekani ya kujikimu na kuchangia padogo kwa Marekani.

Kuwashambulia waziwazi Wasomali walioko Marekani ni mwendelezo wa hivi karibuni wa Trump wa kuwashusha hadhi jamii nzima ya wahamiaji. Wasomali wamehamia Minnesota na majimbo mengine ya Marekani, mara nyingi kama wakimbizi, tangu miaka ya 1990. Aidha, Rais huyo hakutofautisha kati ya Wasomali wenye uraia na wasio raia.

Kauli ya Rais huyo yalikuja siku chache baada ya utawala wake kutangaza kusitisha maamuzi yote ya hifadhi kufuatia kupigwa risasi kwa wanajeshi wawili wa Walinzi wa Kitaifa huko Washington. Mshukiwa wa tukio la wiki jana anatokea Afghanistan lakini Trump ametumia muda huo kuuliza maswali kuhusu wahamiaji kutoka mataifa mengine, ikiwa ni pamoja na Somalia.

"Hawachangii chochote. Siwataki katika nchi yetu," Trump aliwaambia waandishi wa habari karibu na mwisho wa mkutano mrefu wa Baraza la Mawaziri. Aliongeza: " Kuna sababu kwanini nchi yao sio nzuri. Nchi yenu inanuka na hatuwataki katika nchi yetu."

Trump kwa miaka kadhaa amekuwa akimkosoa Mwakilishi wa Bunge la Marekani Ilhan Omar, ambaye alihama kutoka Somalia mwaka 1995 akiwa mtoto.

Hata hivyo Trump alizidisha mashambulizi yake dhidi ya Wasomali kwenye mitandao ya kijamii wiki iliyopita baada ya Christopher Rufo, mwanaharakati wa kihafidhina, kuchapisha madai ambayo hayana uthibitisho katika jarida liitwalo City Journal, akinukuu vyanzo ambavyo havikutajwa, kwamba pesa zilizoibwa kutoka kwa programu za Minnesota zimeenda kwa al-Shabab, kundi la wanamgambo linadhloibiti baadhi ya sehemu za Somalia.