Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema Uturuki inapinga mashambulizi dhidi ya Iran na pia haiungi mkono hatua za kulipiza kisasi za Iran dhidi ya nchi za kanda wakati wa mazungumzo ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Kulingana na vyanzo vya kidiplomasia vya Uturuki, viongozi hao wawili walijadili uhusiano wa mataifa yao mawili pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa siku ya Ijumaa.
Katika mazungumzo hayo, Rais Erdogan pia alionya kuwa mashambulio dhidi ya meli za raia kwenye Bahari Nyeusi yanaharibu utulivu wa kikanda, na kusisitiza kuwa mzozo wa Iran haupaswi kuunda tatizo jipya linaloweza kuathiri mgogoro wa Urusi na Ukraine.
Aidha, Erdogan alisisitiza kuwa sera za uchokozi za serikali ya Israel chini ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu lazima zizuiliwe, na alisisitiza kuwa hatua zinazodhoofisha hadhi ya Jerusalme haziwezi kukubaliwa.



















