| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Anga zafungwa, safari zahairishwa Marekani na Israel zikiishambulia Iran
Israel na Marekani zimeishambulia Iran zikilenga kuizuia kuwa na silaha za nyuklia.
Anga zafungwa, safari zahairishwa Marekani na Israel zikiishambulia Iran
Uamuzi wa kufunga anga, pia ulichukuliwa na Iraq, huku Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu nayo ukisema kuwa itachukua hatua hiyo hiyo./Picha:Wengine
tokea masaa 12

Safari za ndege katika eneo la Mashariki ya Kati zimeendelea kuhairishwa baada ya Marekani na Israel kuishambulia Iran.

Baadhi ya mataifa, yakiwemo Iran, Iraq, Israel, Syria, Kuwait na Umoja wa Falme ya Nchi za Kiarabu, zilitangaza kufunga anga zake, baada ya mashumbulizi hayo, huyu mashirika ya ndege ya Ufaransa, India, Norway, Algeria na Ufaransa yakisitisha safari zake.

Anga zafungwa

Iran nayo ililazimika kufunga anga lake kufuatia mashambulizi hayo.

"Anga yote imefungwa mpaka hapo baadaye," ilisema taarifa ya iliyotolewa na Mamlaka ya Usalama wa Anga ya Iran.

Hali kadhalika, Israel nayo imefunga anga yake, kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Uchukuzi wa nchi hiyo Miri Regev.

Uamuzi wa kufunga anga, pia ulichukuliwa na Iraq, huku Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu nao ukisema kuwa itachukua hatua hiyo hiyo.

CHANZO:AFP