| Swahili
ULIMWENGU
3 dk kusoma
Uingereza na Ufaransa ni miongoni mwa nchi 12 zinazopanga kusitisha biashara na walowezi wa Israel
Mawaziri wa mambo ya nje wamethibitisha mipango ya kuanzisha au kuunga mkono vikwazo vya kitaifa na vya Ulaya dhidi ya bidhaa zinazotoka katika makazi haramu ya Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.
Uingereza na Ufaransa ni miongoni mwa nchi 12 zinazopanga kusitisha biashara na walowezi wa Israel
Mkaazi haramu wa Kiyahudi akitazama kijiji cha Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, ambapo vitendo vya vurugu vya walowezi vimeongezeka.

Nchi 12, zikiwemo Uingereza, Canada na Ufaransa, zimetangaza kuweka vikwazo vya kibiashara dhidi ya walowezi haramu wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, kufuatia kuongezeka kwa mashambulizi yanayofanywa na walowezi hao dhidi ya vijiji vya Wapalestina katika eneo hilo.

Denmark, Finland, Iceland, Ireland, Norway, Poland, Ureno, Hispania na Uswidi pia zinapanga kuweka vikwazo vya kibiashara dhidi ya walowezi haramu wa Isreal, kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumanne na mawaziri wa mambo ya nje wa nchi hizo.

Ireland na Hispania tayari zimechukua hatua dhidi ya kufanya biashara na walowezi haramu wa Israel, huku Ufransa kwa wiki kadhaa ikishinikiza Umoja wa Ulaya kuchukua uamuzi kama huo. Umoja wa Ulaya ni mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Israel, lakini baadhi ya wanachama wamezuia hatua hiyo.

“Vitendo vya serikali ya Israel katika Ukingo wa Magharibi vinadhoofisha suluhisho la mataifa mawili,” mawaziri hao 12 walisema.

Wakiashiria mpango wa kuwa na mataifa mawili—moja la Israel na jingine la Palestina—yakiishi kwa amani bega kwa bega.

“Hali inazidi kuzorota kwa kasi, huku kukiwa na viwango vya ukatili wa walowezi ambavyo havijawahi kushuhudiwa pamoja na upanuzi wa makazi,” walionya.

Mawaziri hao waliongeza: “Serikali ya Israel lazima isimamishe mara moja upanuzi wa makazi na mamlaka za kiutawala za kiraia, ihakikishe kuwa walowezi wanaofanya ukatili wanawajibishwa, na ichunguze madai dhidi ya wanajeshi wa Israel.”

“Kufurushwa kwa misingi ya kikabila”

Mawaziri hao walisema nchi hizo 12 “zinathibitisha nia yao ya kuanzisha hatua za kitaifa na, au kuunga mkono vikwazo vya Ulaya dhidi ya biashara na bidhaa kutoka katika makazi ambayo ni haramu chini ya sheria za kimataifa.”

Waliongeza kuwa baadhi ya nchi hizo pia “zinazingatia kikamilifu hatua hizi na nyingine,” kwa kuzingatia taratibu zao za kitaifa.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Ed Miliband, aliishutumu serikali ya Israel kwa kufumbia macho kile alichokiita “uhamishaji wa lazima kwa misingi ya kikabila” unaofanywa na walowezi haramu katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.

Alisema hatua zilizotangazwa leo “zinatoa ujumbe wa wazi” kwa serikali ya Israel na Wapalestina kwamba: “Hatutakubali kuharibiwa kwa suluhisho la mataifa mawili.”»

Alisema hayo katika taarifa aliyowasilisha kwa wabunge katika Baraza la Wawakilishi la Uingereza.

Miliband alisema kuwa, mbali na sera rasmi ya serikali ya Israel, “ugaidi wa walowezi umeenea kwa kiasi kikubwa.” Aliongeza kuwa Uingereza itaweka vikwazo dhidi ya kundi jingine la walowezi wenye itikadi kali katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, ambao “wameunga mkono au kuchochea vitendo vya vurugu” dhidi ya Wapalestina.

Miliband alisisitiza kwamba watu wanaofadhili au kuwezesha makazi haramu katika Ukingo wa Magharibi “watakabiliwa kikamilifu na vikwazo vya Uingereza.”

Aliendelea kusema kuwa Uingereza itachukua hatua dhidi ya “kampuni na watu binafsi maalumu” wanaotoa huduma na fedha kwa ajili ya upanuzi wa makazi ya Israel yanayochukuliwa kuwa haramu.

Miliband alisema serikali ya Uingereza inakubaliana na kauli kwamba kuna “uhamishaji wa lazima wa Wapalestina kwa misingi ya kikabila” katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, unaofanywa na wale aliowaita “magaidi walowezi” wa Israel.

Katika hotuba yake, pia alithibitisha kwamba usitishwaji wa leseni 30 za kuuza silaha kwa Israel uliowekwa na Uingereza utaendelea “kutekelezwa kikamilifu.”

CHANZO:TRT World and Agencies