| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Kenya ni mwenyeji wa mkutano kati ya Afrika na Ufaransa
Rais William Ruto amesema uamuzi wa kuandaa mkutano huo kwa mara ya kwanza katika nchi isiyozungumza Kifaransa, ni uthibitisho mkubwa wa uhusiano unaokua kati ya nchi hozo mbili.
Kenya ni mwenyeji wa mkutano kati ya Afrika na Ufaransa
Rai wa Ufaransa Emmanuel Macron akipokelewa na Rais wa Kenya William Ruto jijini Nairobi / Reuters

Rais William Ruto wa Kenya Jumapili alimkaribisha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika Ikulu ya Nairobi, kabla ya Mkutano wa siku mbili wa Africa Forward Summit unaoanza leo jijini Nairobi.

Rais William Ruto amesema uamuzi wa kuandaa mkutano huo kwa mara ya kwanza katika nchi isiyozungumza Kifaransa, ni uthibitisho mkubwa wa uhusiano unaokua kati ya nchi hozo mbili.

Ziara ya Macron inajiri wakati Ufaransa inarekebisha sera yake ya Afrika kufuatia kujiondoa kijeshi kutoka mataifa ya Sahel na kugeukia washirika wasio wa Francophone kama Kenya, huku kukiwa na ongezeko la ushindani kutoka kwa mataifa yenye nguvu ya kimataifa kwa ajili ya ushawishi katika bara hilo.

Ziara huku wakosoaji wakihoji uhusiano wa Nairobi na taifa hilo ambalo ni mkoloni wa zamani.

Kenya na Ufaransa tayari zimesaini mikataba ya uboreshaji wa Kituo cha Reli ya Embakasi, mauzo ya chai ya zambarau ya hali ya juu nchini Kenya, matumizi ya amani ya nishati ya nyuklia, na maendeleo ya mradi wa Bwawa la Masinga.

Maeneo mengine ya ushirikiano ni pamoja na uboreshaji wa huduma za hali ya hewa, uzalishaji endelevu wa mafuta ya anga, mabadiliko ya kidijitali, upanuzi wa uwezo wa kuhifadhi makontena kwenye bandari, na uchumi wa buluu na uvuvi.

Rais Ruto aliongeza kusema kuwa Kenya na Ufaransa zimedumisha uhusiano thabiti wa kidiplomasia tangu 1963.

Marais wengine waliowasili kwa ajili ya mkutano huo ni pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa , antonio Gutteres, Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu , Rais Bassirou Diomaye Faye wa Senegal, Jenerali Brice Oligui Nguema ambaye ni Rais wa Gabon.

Pia Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone, Nyuma Boakai wa Liberia na Alassane Ouattara Rais wa Ivory Coast wamehudhuria.

Aziz Akhannouch, Mkuu wa Serikali ya Ufalme wa Morocco na Waziri Mkuu Navinchandra Ramgoolam wa Mauritius pia wako Nairobi kwa mkutano huo wa siku mbili.

CHANZO:TRT Swahili
Soma zaidi
Ronaldo na Messi Kombe la Dunia mara ya 6
"Makubaliano makubwa" yamefikiwa na Iran: Trump
Bajeti ya trilioni 62.33 Tanzania na kupanda kwa gharama ya maisha
Raia 262 wa Nigeria wanaokimbia mashambulizi dhidi ya wageni Afrika Kusini warudishwa nyumbani
Vikosi vya Marekani na Nigeria vyawakata makali zaidi ya magaidi 200 kaskazini mashariki
Mabadiliko ya uchumi Nigeria, Uganda na nchi nyengine za Afrika yamekuza uwekezaji: Benki Kuu
Serikali ya Somalia yasikitishwa na hatua ya kuzuiwa kwa mwamuzi wa nchi hio kuingia Marekani
Watu wasiopungua 12 wauawa katika mashambulizi ya risasi jijini Johannesburg
Refa wa Somalia arudi nyumbani baada ya kukataliwa kuingia Marekani
Trump: Helikopta ya Jeshi la Marekani imedunguliwa na Iran, tutalipiza kisasi
Wakazi wa Afrika Kusini KwaZulu-Natal katika tahadhari baada ya simba kutoroka hifadhi ya wanyama
FIFA yamuondoa mwamuzi kutoka somalia Artan katika Kombe la Dunia baada ya kuzuiwa kuingia Marekani
Waandamanaji wanaopinga kujengwa kwa kituo cha Marekani cha Ebola wakamatwa nchini Kenya
Mwendesha Mashtala wa ICC asimamishwa kazi kwa madai ya dhulma za ngono
Mahakama Kuu ya Kenya: Mchakato wa kumuondoa Gachagua madarakani ulifuata Sheria
Mwamuzi wa kwanza wa Somalia aliyetarajiwa kuchezesha  Kombe la Dunia azuiwa kuingia Marekani
Uhamiaji: Afrika Kusini kuhamisha vituo vya wakimbizi hadi maeneo ya mpakani
Davido, Burna Boy, Rema na Tyla kutumbuiza Kombe la Dunia 2026
Mauritius yakataa pendekezo lililoripotiwa la Marekani la kununua Visiwa vya Chagos
Wananchi waelimishwe kuhusu umuhimu wa kuandikishana mikataba ya ardhi-Wazri Mkuu wa Tanzania