tokea masaa 4
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kupiga kura siku ya Jumanne kuhusu azimio la kulinda meli za kibiashara katika Mlango-Bahari wa Hormuz.
Kura hiyo imepangwa kufanyika saa 12 jioni saa za Afrika Mashariki (15:00) GMT, saa chache kabla ya muda wa mwisho uliotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump kwa Iran kukubali makubaliano au miundombinu yake kushambuliwa.
Bei ya mafuta imepanda tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran mwishoni mwa mwezi wa Februari yaliposababisha mzozo ambao umesababisha msongamano wa meli kwenye Mlango Bahari, njia ambayo hupitisha takriban theluthi moja ya nishati duniani
CHANZO:TRT World
















