| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Ndege ya Ethiopia yazuiwa kutua Israel kutokana na uraia wa rubani
Hii ni baada ya kubainika kuwa, rubani wa ndege hiyo alikuwa ni raia wa Indonesia.
Ndege ya Ethiopia yazuiwa kutua Israel kutokana na uraia wa rubani
Hii ni baada ya kubainika kuwa, rubani wa ndege hiyo alikuwa ni raia wa Indonesia.

Ndege ya mizigo inayomilikiwa na shirika la Ethiopia, ikitokea Addis Ababa kuelekea Tel Aviv, ililazimika kurudia angani baada ya Israel kuinyima kibali cha kutua nchini humo.

Hii ni baada ya kubainika kuwa, rubani wa ndege hiyo alikuwa ni raia wa Indonesia.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Oktoba 12, 2026, baada ya ndege hiyo kuondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bole, Addis Ababa.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Israel, orodha ya wafanyakazi wa ndege hiyo iliwasilishwa kwa mamlaka husika baada ya safari kuanza.

Baada ya kubaini uraia wa rubani huyo, mamlaka za Israel ziliizuia ndege hiyo kuingia katika anga lake. Ndege hiyo ilirejea Addis Ababa baada ya kumwaga sehemu ya mafuta juu ya bahari, kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa.

Rubani huyo alibadilishwa na mwingine aliyeidhinishwa, na ndege ikaendelea na safari yake hadi Israel bila tukio jingine.

Kwa sasa, Israel na Indonesia hazina uhusiano wowote wa kidiplomasia.

Tukio hilo, limetokea chini ya wiki mbili, baada ya ndege ya Flydubai, iliyokuwa ikitoka Dubai kuelekea Tel Aviv, kulazimika kubadili njia na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Tabuk, Saudi Arabia, baada ya kuripotiwa kutokea ugomvi kati ya marubani ndani ya chumba chao.

CHANZO:TRT Afrika Swahili