Spika wa Bunge la Uturuki ataka Israel iondolewe Umoja wa Mataifa

Numan Kurtulmus ametaka Israel isitishiwe uanachama wake kufuatia kupitishwa kwa hukumu ya kifo kwa wafungwa wa Palestina.

By
Spika wa Bunge la Uturuki Numan Kurtulmus./Picha:AA

Spika wa Bunge la Uturuki Numan Kurtulmus ametaka Israel isitishiwe uanachama wake ndani ya Umoja wa Mataifa, akitoa sababu ya kupitishwa kwa hukumu ya kifo dhidi ya Wapalestina.

Akizungumza wakati mkutano wa 152 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) unaofanyika jijini Istanbul, Kurtulmus alibainisha kuwa, jumuiya ya kimataifa iliwahi kuchukua hatua dhidi ya utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini, kwa kuivua uanachama taifa hilo mwaka 1974.

"Je, hukumu hiyo hailengi kuwabagua Wapalestina?” alihoji Spika huyo.

Katika hatua nyingine, Kurtulmus ameukosoa Umoja wa Mataifa, akisema kuwa ulishindwa kuzuia migogoro inayoendelea ulimwenguni, ukiwemo ule wa Gaza.

"Kwa bahati mbaya, Umoja wa Mataifa umekuwa taasisi yenye kusikiliza maslahi ya waliopo madarakani," alibainisha.

Wito wa mageuzi

Kulingana na Kurtulmus, mataifa yote ulimwenguni yana haki sawa.

Wakati wa mkutano huo, Spika huyo alipata fursa ya kukutana Mwenyekiti wa Baraza la Shura la Oman Khalid Al Maawali, na kumshukuru kwa jitihada zake za usuluhishi, akitoa wito wa kufufuliwa kwa mazungumzo ya Pakistan.

Pia, alionya matendo ya Israel yanahatarisha mgogoro kati ya nchi za Guba na taifa la Iran.