| Swahili
MICHEZO
2 dk kusoma
Ubaguzi wa rangi: Wachezaji wanaoziba mdomo wanaweza 'kuoneshwa kadi nyekundu'
Hatua hii inaweza kuanza kuchukuliwa katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka huu.
Ubaguzi wa rangi: Wachezaji wanaoziba mdomo wanaweza 'kuoneshwa kadi nyekundu'
Prestianni anakanusha madai ya kusema maneno ya ubaguzi wa rangi dhidi ya Vinicius / AFP / AFP
tokea masaa 15

Rais wa shirikisho la soka duniani FIFA Gianni Infantino amesema kuhusu uwezekano wa kuonesha kadi nyekundu wachezaji ambao wanaziba midomo wakati wakiwakabili wapinzani wao.

Hali hii imedhihirika katika wiki za hivi karibuni baada ya mchezaji wa Real Madrid Vinicius Junior kusema kuwa alitukanwa kwa misingi ya ubaguzi wa rangi na mchezaji wa Benfica Gianluca Prestianni wakati wa mechi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Prestianni, ambaye anakanusha madai hayo, alimsogelea Vinicius akiwa amefunika mdomo wake na jezi ambapo Madrid ilipata ushindi wa 1-0 katika mechi yake ya mkondo wa kwanza ya hatua ya mtoano. Amepigwa marufuku kucheza mechi ya mkondo wa pili huku uchunguzi ukiendelea.

Suala la wachezaji kuziba midomo yao lilijadiliwa siku ya Jumamosi katika mkutano Bodi ya Kimataifa ya Soka (IFAB).

Hatua hiyo inaweza kuanza kuchukuliwa wakati wa mechi za Kombe la Dunia mwaka huu.

“Kama mchezaji ataziba mdomo na kusema kitu, na hii matokeo yake ni ubaguzi wa rangi, basi inabidi aoneshwe kadi nyekundu,” Infantino aliiiambia Sky News. “Tutadhani kuwa kuwa amesema kitu ambacho hakutakiwa kusema; la sivyo, hakutakiwa kuziba mdomo.

“Sielewi kwa nini – kama huna cha kuficha, hutakiwi kuziba mdomo wako wakati unazungumza.

“Ndiyo hivyo, hamna mjadala. Na hizi ndizo hatua tutakazochukua, na inabidi tuchukue hatua hizi madhubuti kwa vita vyetu dhidi ya ubaguzi wa rangi.”

CHANZO:TRT Afrika Swahili