Mahakama Kuu ya mjini Durban imekataa ombi la Duduzile Zuma-Sambudla, binti wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma, la kutaka mashtaka yanayohusiana na ugaidi dhidi yake kuondolewa.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Mei 2027, huku Zuma-Sambudla akiwa nje kwa kupewa onyo, shirika la habari la taifa SABC limeripoti.
Anakabiliwa na mashtaka ya uchochezo ya kutekeleza ugaidi na vurugu kwa umma kutokana na ujumbe katika mitandao ya kijamii yanayohusishwa na vurugu za Julai 2021.
Waendesha mashtaka wanadai kuwa Zuma-Sambudla alihusika katika kuhamasisha vurugu kwa ujumbe wake mitandaoni na picha wakati wa vurugu hizo, madai ambayo anakanusha.
Utetezi
Upande wa utetezi, unaoomngozwa na Wakili Dali Mpofu, unaeleza kuwa serikali imeshindwa kutoa ushahidi wa kutosha kubaini yaliyomo kwenye mashtaka hayo. Mpofu pia alihoji kama ujumbe katika mitandao ya kijamii unasababisha uchochezi usi halali na kudai kuwa analengwa kutokana na jina lake la mwisho.
Mwendesha mashtaka wa umma Wakili Mayen Naidoo alisisitiza kuwa upande wa mashtaka umetoa ushahidi wa kutosha, akieleza kuwa muendelezo wa ujumbe mitandani na lugha iliotumika inaweza kutafsiriwa kuwa kuhamasisha vurugu.





















