Erdogan: Mipango yote ya kutafuta amani ya Gaza ni ya umuhimu
Akizungumza kwa njia ya simu na kiongozi mwenzake wa Brazil, rais wa Uturuki amefurahishwa na hatua ya Brazil kutokukaa kimya kufuatia mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza.
Uturuki inazingatia hatua zote za kutafuta amani katika eneo la Gaza kuwa ni za uhumimu, amesema Rais Recep Tayyip Erdogan wakati wa mazungumzo yake kwa njia ya simu na Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil.
Erdogan, pia ameonesha kufurahishwa na hatua ya Brazil kutokukaa kimya, huku mauaji ya kimbari ya Israel dhidi ya Gaza yakiendelea.
Katika mazungumzo hayo, wawili hao walijadiliana uhusiano wa nchi mbili, kikanda na masuala mengine ya ulimwengu, kulingana na taarifa ya Kurygenzi ya Mawasiliano ya Uturuki kupitia mtandao wa kijamii wa Uturuki wa NSosyal siku ya Jumatano.
Kulingana na Erdogan, Ankara itaendelea na jitihada za kumaliza majanga ya kibinadamu katika eneo la Gaza.
Rais huyo wa Uturuki amesisitiza azma ya kufanya kazi kwa pamoja katika kukuza ushirikiano.
Israel imeua zaidi ya Wapalestina 71,000 na kujeruhi wengine zaidi ya 171,000, ikiharibu asilimia 90 ya miondombinu ya Gaza kuanzia Oktoba 2023.