Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) limependeza mabadiliko makubwa ya sheria ya kadi za njano kuelekea michuano ya Kombe la Dunia 2026, ambayo itaanza siku 45 zijazo.
Lengo la mabadiliko hayo, ni kuzuia wachezaji kukosa mechi muhimu, kwa kuwa na kadi za njano zaidi ya moja.
Katika kikao chake ambacho kitaketi Aprili 28, 2026, baraza la maamuzi la FIFA, limependekeza kufutwa kwa zote za njano atakazopata mchezaji baada ya hatua ya makundi maarufu kama hatua ya mtoano, na baada ya hatua ya Robo Fainali.
Mabadiliko haya, yanakuja wakati ambapo michuano ya mwaka huu, itashuhudia ongezeko la timu zitakazoshiriki mashindano hayo makubwa duniani.
Michuano ya mwaka huu, ambayo inaandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico, itakuwa na jumla ya timu 48 badala ya 32, kama ilivyozoeleka awali, na hivyo kuwalazimu wachezaji kucheza mechi nyingi zaidi kufikia fainali.
Michuano ya Kombe la Dunia inatarajiwa kuanza Juni 11 na kumalizika Julai 19, 2026.














